Guadeloupe
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Guadeloupe | |||
| Mahali pa Guadeloupe na Ufaransa | |||
|
|||
| Nchi | |||
|---|---|---|---|
| Mji mkuu | Basse-Terre | ||
| Eneo | |||
| - Mkoa | 1,628 km² | ||
| Tovuti: http://www.cr-guadeloupe.fr/ | |||
Guadeloupe ni eneo la ng'ambo na mkoa (departement)wa Ufaransa katika Bahari ya Karibi lenye visiwa tisa vidogo. Mji mkuu ni Basse-Terre.
Wakazi asilia walikuwa Waindio. Utamaduni wao uliharibiwa kabisa kwa kuja kwa ukoloni wa Ulaya. Ikawa koloni ya Ufaransa halafu ya Uingereza halafu ya Uswidi halafu ya Ufaransa tena.
Eneo lake ni 1,780 km². Idadi ya wakazi ni takriban lakhi 4 na nusu. Asilimia 90 za wakazi ni wa asili ya Kiafrika ikiwa wazee wao walipelekwa hapa kama watumwa kwa ajili ya kazi za mashamba ya miwa.
Tazama pia [hariri]
- Martinique ni eneo nyingine ya Ufaransa katika Bahari ya Karibi.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guadeloupe kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |