Honduras

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
República de Honduras
Jamhuri ya Honduras
Bendera ya Honduras Nembo ya Honduras
Bendera Nembo
Wito la taifa: Libre, Soberana e Independiente
Wimbo wa taifa: „Tu bandera es un lampo de cielo“
(wewe bendera u nuru ya angani)
Lokeshen ya Honduras
Mji mkuu Tegucigalpa
14°6′ N 87°13′ W
Mji mkubwa nchini Tegucigalpa
Lugha rasmi Kihispania
Serikali Jamhuri, demokrasia
Juan Orlando Hernández
Uhuru
Imetangazwa
imetambuliwa

15 Septemba 1821
1823
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
112,492 km² (ya 102)
(kidogo sana)
Idadi ya watu
 - Julai 2006 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
7,326,496 2 (ya 96)
6,975,204
64/km² (ya 128)
Fedha Lempira (HNL)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-6)
(UTC)
Intaneti TLD .hn
Kodi ya simu +504

-Honduras ni nchi ya Amerika ya Kati. Imepakana na Guatemala, El Salvador na Nikaragua. Upande wa kusini ina pwani fupi la Pasifiki na upande wa kaskazini pwani ndefu la Bahari ya Karibi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Ramani ya Honduras

Honduras ni nchi ya milima mingi inayopanda hadi kimo cha Cerro Las Minas chenye 2849 m juu ya UB.

Hali ya hewa ni kitropiki lakini joto inapoa milimani.

Miji[hariri | hariri chanzo]

Mji mkuu na mji mkubwa mwenye wakazi milioni 1.09 ni [Tegucigalpa]]. Miji minhine mikubwa kiasi ni San Pedro Sula (wakazi 491,000) katika kaskazini-magharibi, halafu miji ya bandari ya La Ceiba (wakazi 111,000) na Puerto Cortés (wakazi 36,000).

Mito na maziwa[hariri | hariri chanzo]

Mito mingi ya Honduras huelekea Atlantiki. Río Patuca na Río Ulúa ni mito mirefu ya nchi. Ziwa kubwa la Lago de Yojoa lenye eneo la 285 km² ni muhimu kwa ajili ya ajili ya maji ya miji.

Kanisa Kuu la Tegucigalpa lilijengwa wakati wa utawala wa Hispania

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya wakazi ni takriban milioni 14 hivyo ni nchi yenye wakazi wengi katika Amerika ya Kati. Wakazi walio wengi wengi kabisa ni machotara hasa wenye asili ya mchanganyiko wa wazalendo na Wazungu. Hao ndio aslilima 90 ya wakazi. Katika misitu ya milimani kuna bado vikundi vya wenyeji asilia (Wahindi wekundu). Wengine ni wa asili ya Afrika au ya Ulaya wasiochanganyika sana na wengine. Kwneye pwani la kaskazini kuna makazi ya Wagarifuna ambao ni utamaduni wa mchanganyiko wa Wahindi wekundu na Waafrika.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Honduras ilikuwa sehemu ya maeneo ya Wamaya. Lakini miji yao ilikwaisha tayari kabla ya kufika kwa Wahispania. Kristoforo Kolombo alifika mwaka 1502 karibu na Trujillo katika kaskazini na kuita nchi "Honduras" (=Kihisp. vilindi) kwa sababu ya maji marefu mwambanoni.

1524/1525 Wahispania walianza kuvamia nchi na kuunda mji wa Comayagua mwaka 1540. Mji mkuu wa leo ulianzishwa mwaka 1579 kama kituo cha kuchimba madini kama dhahabu na fedha.

1821 Honduras ilijiunga na ghasia ya maeneo mengine ya Amerika ya Kati dhidi ya utawala wa Hispania. Mwanzoni nchi hizi ndogo zilijiunga na Meksiko lakini baada ya miaka miwili zilianzisha "Shirikisho la Amerika ya Kati" iliyokwisha mwaka 1839. Tangu mwaka ule Honduras imekuwa nchi ya kujitegemea kabisa.

Centroamerica politico.png Makala hii kuhusu maeneo ya Amerika ya Kati bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Honduras kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

SIASA HONDURAS[hariri | hariri chanzo]

Kwa mnamo leo Raisi wa Honduras anaitwa Porfirio Lobo Sosa.Raisi ndiye kiongozi wa Nchi na pia serikali.ishitoshe yeye ndiye pia amri njeshi mkuu.