Tropiki
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tropiki ni kanda la dunia lililopo pande zote mbili za ikweta kati ya latitudo za 23.5° za kaskazini na za kusini.
Ni kanda la joto duniani. Hapa jua linafikia mahali pa juu kabisa angani hivyo kanda hili linapokea mwanga na joto zaidi. Katika maeneo kusini na kaskazini yake jua halifiki kamwe juu kabisa.
Pia hakuna tofauti kubwa katika muda wa mchana na usiku jinsi ilivyo nje ya tropiki kuelekea nchani. Hii ni pia sababu ya kwamba nchi za tropiki hazijui majira kama maeneo yenye joto ya wastani au maeneo karibu na ncha za dunia.

