Wikipedia:Matukio ya hivi karibuni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Makala ya 79,000[hariri chanzo]

Tarehe 9 Desemba 2023 Wikipedia hii imefikia makala ya 79,000 kwa ukurasa juu ya kata ya Chemchem (Unguja) katika mradi wa kata mpya za Tanzania.


Kipala
Amekufa 10 Julai 2023
Nchi Ujerumani
Kazi yake Mchungaji
Cheo Mchungaji

Kifo cha Kipala[hariri chanzo]

Tarehe 10 Julai 2023 mwenzetu bureaucrat Kipala ameaga dunia. Mchungaji wa Kilutheri na mmisionari katika nchi mbalimbali, zikiwemo Tanzania, Kenya na Iran, Ingo Koll amefariki nyumbani mwake nchini Ujerumani. Alichangia sana kamusi elezo ya lugha yetu tangu tarehe 13 Machi 2006 hadi tarehe 28 Juni 2023. Mbali ya hilo, alikuwa kiungo kikuu katika kutuweka pamoja kama Wikipedia ya Kiswahili. Alitoa mchango mkubwa sana katika kuistawisha na katika mijadala mbalimbali, pamoja na kutuwakilisha kimataifa. Mwenyezi Mungu amjalie raha ya milele. Amina.

Tarehe 13 Mei 2023 alikuwa amemuandikia ndugu Rikardo: "Juzi daktari aliniarifu kwamba nimepata kansa. Aina hiyo kwenye kongosho inaweza kuendelea haraka sana, lakini kuna uwezekano fulani wa tiba itakayoongeza muda kidogo ... labda mwaka 1 au miwili. Hadi sasa sisikii matatizo lakini nahisi maumivu yatakuja, na matokeo ya tiba ya madawa makali yataniathiri pia. Kwa hiyo - sijui sasa nitaweza kuendelea kwa muda gani. Wiki ijayo naingia hospitalini kwa utafiti zaidi.

Sidhani ni wakati wa kuaga sasa. Sina hamu ya kupokea wimbi la "pole". Tangu nimepita umri wa miaka 70 nilijiambia "kuanzia sasa hakuna cha kulalamika", maana katika kazi yangu nimezika watu mamia nilipenda kusoma zaburi ya 90. Nachukua wakati wangu kama zawadi. Sikutegemea nitapatwa na kansa ya haraka vile lakini sioni faida ya kulalamika. Hadi sasa maisha yangu yamekuwa mazuri sana, nina kila sababu kumshukuru Mungu na kushukuru watu niliokuta kwenye njia zangu. Hii ni pamoja na wewe!"

Makala ya 78,000[hariri chanzo]

Tarehe 15 Juni 2023 Wikipedia hii imefikia idadi ya 78,000 kwa makala juu ya Jamil Adam katika mradi wa wachezaji wa mpira wa miguu.

Makala ya 77,000[hariri chanzo]

Tarehe 25 Machi 2023 Wikipedia hii imefikia idadi ya 77,000 kwa makala juu ya Chomutov, mji wa Ucheki.

Wakabidhi wapya wanne[hariri chanzo]

Mwezi Aprili 2023 ulifanyika uchaguzi wa wakabidhi wapya. Kati ya 6 waliogombea, 4 wamechaguliwa kwa kupata zaidi ya nusu ya kura halali. Kazi njema, ndugu!

Makala ya 76,000[hariri chanzo]

Tarehe 23 Desemba 2022 Wikipedia hii imefikia idadi ya 76,000 kwa makala juu ya Bouhjar, mji wa Tunisia.

Makala ya 75,00[hariri chanzo]

Tarehe 17 Septemba 2022 Wikipedia hii imefikia idadi ya 75,000 kwa makala juu ya Kouandé, mji wa Benin.

Makala ya 74,00[hariri chanzo]

Tarehe 15 Julai 2022 Wikipedia hii imefikia idadi ya 74,000 kwa makala juu ya Ghuba ya Venezuela.

Makala ya 73,00[hariri chanzo]

Tarehe 6 Juni 2022 Wikipedia hii imefikia idadi ya 73,000 kwa makala juu ya Frenda, mji wa Algeria.

Makala ya 72,00[hariri chanzo]

Tarehe 14 Mei 2022 Wikipedia hii imefikia idadi ya 72,000. Kwa kuwa makala nyingi zimetungwa kwa mashindano, kuna kazi kubwa ni kuziweka sawa.

Makala ya 71,00[hariri chanzo]

Tarehe 23 Aprili 2022 Wikipedia hii imefikia idadi ya 71,000 kwa makala nyingi za mradi wa.

Makala ya 70,00[hariri chanzo]

Tarehe 10 Machi 2022 Wikipedia hii imefikia idadi ya 70,000 kwa makala juu ya Ilesa katika mradi wa miji ya Nigeria.

Makala ya 69,000[hariri chanzo]

Tarehe 11 Januari 2022 Wikipedia hii imefikia idadi ya 69,000 kwa makala juu ya Maroua katika mradi wa miji ya Kamerun.

Makala ya 68,000[hariri chanzo]

Tarehe 29 Oktoba 2021 Wikipedia hii imefikia idadi ya 68,000 kwa makala juu ya Chambishi katika mradi wa miji ya Zambia.

Makala ya 67,000[hariri chanzo]

Tarehe 9 Septemba 2021 Wikipedia hii imefikia idadi ya 67,000 kwa makala juu ya Nairagie Ngare katika mradi wa vijiji vya Kenya.

Makala ya 66,000[hariri chanzo]

Tarehe 14 Agosti 2021 Wikipedia hii imefikia idadi ya 66,000 kwa makala juu ya Makutano katika mradi wa kata za Kenya.

Makala ya 65,000[hariri chanzo]

Tarehe 5 Julai 2021 Wikipedia hii imefikia idadi ya 65,000 kwa makala juu ya Mwea katika mradi wa kata za Kenya.

Makala ya 64,000[hariri chanzo]

Tarehe 19 Juni 2021 Wikipedia hii imevuka idadi ya 64,000 kutokana na tendo la kurudisha makala 907 lililofanywa na steward aliyekuwa amezifuta kwa mkupuo mmoja mwaka 2020.

Makala ya 63,000[hariri chanzo]

Tarehe 8 Juni 2021 mradi wa Africa Wiki Challenge Arusha kuhusu viwanja vya michezo umefikisha Wikipedia yetu hadi kutunga makala ya 63,000 na kusonga mbele haraka. Hongera na asante kwa wahusika wote! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:58, 9 Juni 2021 (UTC)[jibu]

Makala ya 62,000[hariri chanzo]

Tarehe 7 Mei 2021 mradi wa miji ya Italia umefikisha Wikipedia yetu kwenye makala ya 62,000 kwa ukurasa juu ya San Giovanni Rotondo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:28, 7 Mei 2021 (UTC)[jibu]

Makala ya 61,000[hariri chanzo]

Tarehe 15 Machi 2021 mradi wa watakatifu Wakristo umefikisha Wikipedia yetu kwenye makala ya 61,000 kwa ukurasa juu ya Agrikola wa Chalon. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:19, 15 Machi 2021 (UTC)[jibu]

Makala ya 60,000[hariri chanzo]

Tarehe 20 Agosti 2020 mradi wa mito ya Burundi umefikisha Wikipedia yetu kwenye makala ya 60,000 kwa ukurasa juu ya Mto Rubirizi (Muramvya). --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:28, 20 Agosti 2020 (UTC) Tarehe 8 Novemba 2020 Wikipedia yetu imetimiza tena idadi hiyo baada ya kukatwa makala 800 hivi hapo katikati (mpaka sasa hatujajua ilikuwaje). Ukurasa husika ni juu ya mtakatifu Andrea Avellino. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:14, 8 Novemba 2020 (UTC)[jibu]

Makala ya 59,000[hariri chanzo]

Tarehe 22 Mei 2020 mradi wa miji ya Rwanda umefikisha Wikipedia yetu kwenye makala ya 59,000 kwa ukurasa juu ya Mukarange. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:02, 22 Mei 2020 (UTC)[jibu]

Makala ya 58,000[hariri chanzo]

Tarehe 3 Aprili 2020 mradi wa mito ya Burundi umefikisha Wikipedia yetu kwenye makala ya 58,000 kwa ukurasa juu ya Mto Gihororo (Karuzi). --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:55, 3 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Makala ya 57,000[hariri chanzo]

Tarehe 17 Machi 2020 mradi wa wachezaji mpira umefikisha Wikipedia yetu kwenye makala ya 57,000 kwa ukurasa juu ya Gilmar Rinaldi. Kurasa elfu kwa juma moja tu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 05:44, 18 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Makala ya 56,000[hariri chanzo]

Tarehe 10 Machi 2020 mradi wa Makabila ya Uganda umefikisha Wikipedia yetu kwenye makala ya 56,000 kwa ukurasa juu ya Wakumam. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:36, 10 Machi 2020 (UTC)[jibu]

Makala ya 55,000[hariri chanzo]

Tarehe 13 Desemba 2019 mradi wa Watakatifu wa Afrika umefikisha Wikipedia yetu kwenye makala ya 55,000 kwa ukurasa juu ya Yusto askofu. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:17, 13 Desemba 2019 (UTC)[jibu]

Makala ya 54,000[hariri chanzo]

Tarehe 4 Oktoba 2019 makala ya 54,000 imetungwa kuhusu wafiadini wa Afrika Suksesi na wenzake 17. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:23, 4 Oktoba 2019 (UTC)[jibu]

Makala ya 53,000[hariri chanzo]

Tarehe 10 Agosti 2019 makala ya 53,000 imetungwa kuhusu Tarafa ya Tiémélékro. Tunawashukuru wachangiaji wetu kutoka Cote d'Ivoire. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:58, 11 Agosti 2019 (UTC)[jibu]

Makala ya 52,000[hariri chanzo]

Tarehe 16 Julai 2019 makala ya 52,000 imetungwa kuhusu mto Rwoho. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:55, 16 Julai 2019 (UTC)[jibu]

Makala ya 51,000[hariri chanzo]

Tarehe 31 Mei 2019 makala ya 51,000 imetungwa kuhusu mto Osia. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:35, 31 Mei 2019 (UTC)[jibu]

Makala ya 50,000[hariri chanzo]

Tarehe 3 Mei 2019 makala ya 50,000 imetungwa kuhusu mto Ocere. Hatimaye tumefikia hatua hiyo kubwa! Hongera kwa wote! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:31, 3 Mei 2019 (UTC)[jibu]

Makala ya 49,000[hariri chanzo]

Tarehe 23 Machi 2019 makala ya 49,000 imetungwa kuhusu mto Wangodugu. Tukazane ili kufikia mapema ya 50,000! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:12, 23 Machi 2019 (UTC)[jibu]

Hongera sana Ndugu Riccardo kwa michango yako!! Na asante!Kipala (majadiliano) 19:58, 23 Machi 2019 (UTC)[jibu]

Makala ya 48,000[hariri chanzo]

Tarehe 7 Februari 2019 makala ya 48,000 imetungwa kuhusu kisiwa cha Musira. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:30, 7 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Makala ya 47,000[hariri chanzo]

Tarehe 8 Novemba 2018 makala ya 47,000 imetungwa kuhusu mto Olkimatare. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:26, 8 Novemba 2018 (UTC)[jibu]

Makala ya 46,000[hariri chanzo]

Tarehe 15 Oktoba 2018 makala ya 46,000 imetungwa kuhusu mto Wakavi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:41, 15 Oktoba 2018 (UTC)[jibu]

Ukurasa wa 100,000[hariri chanzo]

Tarehe 5 Oktoba 2018, kwa makala juu ya Mto Thiririka, Wikipedia yetu imefikia ukurasa wa 100,000 zikihesabiwa si makala tu, bali pia kurasa za maelekezo, majadiliano, watumiaji n.k. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:41, 5 Oktoba 2018 (UTC)[jibu]

Baba Tabita kuaga[hariri chanzo]

Tarehe 26 Septemba 2018, huyo mchangiaji wetu mkuu ameandika ili kutuaga baada ya kazi ya miaka 12 na kisha kuugua kwa muda mrefu, akisema hajui kama ataweza kuchangia tena. Tunazidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu aweze kupona na kuendelea nasi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:31, 26 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Makala ya 45,000[hariri chanzo]

Tarehe 12 Agosti 2018 makala ya 45,000 imetungwa kuhusu mto Ilangi, korongo wa Kenya. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:11, 12 Agosti 2018 (UTC)[jibu]

Makala ya 44,000[hariri chanzo]

Tarehe 30 Julai 2018 makala ya 44,000 imetungwa kuhusu mto Nyairoko. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:55, 30 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Makala ya 43,000[hariri chanzo]

Tarehe 7 Julai makala ya 43,000 imetungwa kuhusu mto Kaptarit. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:36, 7 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Makala ya 42,000[hariri chanzo]

Tarehe 21 Mei 2018, makala ya 42,000 imetungwa kuhusu mto Jigulu. Mbele kwa mbele! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:18, 21 Mei 2018 (UTC)[jibu]

Makala ya 41,000[hariri chanzo]

Tarehe 2 Mei 2018, makala ya 41,000 ilianzishwa na Ndugu Riccardo kuhusu Mto Ligunga. Tusonge mbeleee! --Baba Tabita (majadiliano) 05:13, 3 Mei 2018 (UTC)[jibu]

Ninja Ndugu Riccardo katika ubora wake. Safi sana! Tunasonga. Sasa hivi tutafika walipo Afrikaans!--Muddyb Mwanaharakati Longa 08:22, 3 Mei 2018 (UTC)[jibu]

Makala ya 40,000[hariri chanzo]

Tarehe 17 Machi 2018, makala ya 40,000 (AROBAINI ELFU, jamani!) ni kuhusu mlima Nidze. Makala ilianzishwa na Ndugu Riccardo. Asante na hongera, Mzee! Sherehe itafanyika wapiii? Tupo pamoja katika furaha na fahari. --Baba Tabita (majadiliano) 09:52, 17 Machi 2018 (UTC)[jibu]

Sasa niseme tu, zama zangu zimeisha! Nyakati zangu nilipiga buku ndani ya wiki 2. Furaha iliyopo hadi mgonjwa umeamka kitandani. Pole sana mzee wangu, Oliver, na ahsante kwa taarifa!--MwanaharakatiLonga 12:37, 17 Machi 2018 (UTC)[jibu]
Kweli tunahitaji sherehe. Hongereni ndugu zangu wote! --Ndesanjo (majadiliano) 23:44, 30 Mei 2018 (UTC)[jibu]

Makala ya 39,000[hariri chanzo]

Tarehe 24 Desemba 2017, makala ya 39,000 imeandikwa. Sasa tunalenga ya 40,000: tujitahidi pamoja. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:48, 13 Januari 2018 (UTC)[jibu]

Makala ya 38,000[hariri chanzo]

Tarehe 12 Oktoba 2017, makala ya 38,000 ni kuhusu Ziwa Kamnarok, ziwa lililokauka la Kenya. Makala iliandikwa na Ndugu Riccardo. --Baba Tabita (majadiliano) 21:16, 13 Oktoba 2017 (UTC)[jibu]

Makala ya 37,000[hariri chanzo]

Tarehe 30 Julai 2017, makala ya 37,000 ni kuhusu Ziwa Ambussel, ziwa dogo la Tanzania. Makala iliandikwa na Ndugu Riccardo. --Baba Tabita (majadiliano) 17:44, 30 Julai 2017 (UTC)[jibu]

Makala ya 36,000[hariri chanzo]

Tarehe 20 Mei 2017, makala ya 36,000 ni kuhusu Abdallah Majurah Bulembo, mwanasiasa wa Tanzania. Makala iliandikwa na Ndugu Luhazi. --Baba Tabita (majadiliano) 18:29, 20 Mei 2017 (UTC)[jibu]

Makala ya 35,000[hariri chanzo]

Tarehe 12 Januari 2017, makala ya 35,000 ni kuhusu mwandishi James Tate aliyepokea Tuzo ya Pulitzer ya Ushairi mwaka wa 1992. --Baba Tabita (majadiliano) 10:41, 12 Januari 2017 (UTC)[jibu]

Makala ya 33,000[hariri chanzo]

18 Aprili 2016, makala ya 33,000 ni Kio'du, lugha ya Vietnam na Laos. --Baba Tabita (majadiliano) 11:43, 18 Aprili 2016 (UTC)[jibu]

Haririo la 1,000,000[hariri chanzo]

Upande wa maharirio, tarehe 10 Oktoba 2015 yamefikia idadi ya milioni 1.

Makala ya 30,000[hariri chanzo]

Nimejitahidi lakini nahisi aliyepita ni Riccardo mnamo tar. 21. Septemba 2015, sina uhakika makala gani. Kipala (majadiliano) 21:32, 23 Septemba 2015 (UTC)[jibu]

Ni Historia ya Madagaska tarehe 22 Septemba 2015. Hongera kwa wote! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:55, 24 Septemba 2015 (UTC)[jibu]

Makala ya 29,000[hariri chanzo]

  • 13 Juni 2015, makala ya 29,000 ni Pembe kuu‎ (pembe ya 180°, isiyoonekana kama pembe inafanana na mstari wa kawaida...)

Warsha ya Wikipedia Morogoro[hariri chanzo]

Tarehe 21 Machi 2015, wahariri wafuatao walitoa warsha ya kuandika na kuhariri makala za wikipedia ya Kiswahili kwa walimu na wanafunzi wa shule ya sekondari ya AlfaGems mjini Morogoro: Riccardo Riccioni, Kipala, ChriKo na Baba Tabita (bahati mbaya, Muddyb Blast Producer alibanwa kazini na kutoweza kuhudhuria). Tumefurahi kuona mafanikio mema!

Makala ya 28,000[hariri chanzo]

Makala ya 22,000[hariri chanzo]

  • 28 Oktoba 2011 imefika makala 22,000!

Makala ya 20,000[hariri chanzo]

Makala ya 15,000[hariri chanzo]

  • 25 Desemba 2009 (UTC)  :-)

Mlimba ni tarafa iliyopo katika wilaya ya Kilombero katika Mkoa wa Morogoro. Ipo umbali wa kilomita 150 kutoka Ifakara mjini. Tarafa ya Mlimba ina ujumla wa kata 6. Kata ya Tanganyika Masagati ni kata maarufu sana katika tarafa ya Mlimba. Ipo umbali usiopungua kilomita 100 kutoka Mlimba mjini. Tarafa hii inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ya usafiri, utumishi wa umma {walimu,madaktari n.k}. Wakazi wa mlimba wanategemea zaidi usafiri wa TAZARA. Kata ya Mlimba ina shule za msingi zisizopungua 10 na sekondari 3.Tarafa ya Mlimba ina shule zaidi ya 30 za msingi na 8 za sekondari. Moja kati ya shule maarufu ni shule ya msingi MAKIRIKA na shule ya sekondari MLIMBA GIRLS. Shule ya msingi MAKIRIKA ipo umbali wa kilomita 10 kutoka Mlimba mjini. Shule hii ipo katika kijiji cha Makirika. Ina walimu 4 {Donatus Dacky, Abel Michael, John Justine na Selemani Mkonje},shule ina darasa la awali hadi la saba! Pia katika tarafa ya mlimba utakutana na mgodi wa umeme{KIHANSI}... imehaririwa na selemani mkonje

Maendeleo ya makala za kata nchini Tanzania[hariri chanzo]

Makala za kata zinafuata majina ya kata yaliyotajwa katika taarifa ya sensa 2002. Kata zilizoanzishwa baadaye kwa kawaida hazipo bado. Kata zote za Tanzania zimepata makala fupi ya mbegu; mengine yameshapanushwa. Ilikuwa kazi kubwa na ya maana!

Kazi inayobaki ni kufuatilia habari za wilaya mpya zilizoanzishwa mwaka 2006/2007 kwa sababu orodha ya kata iliyopatikana ilikuwa ya sensa ya mwaka 2002. Pale tulipotambua wilaya mpya tulianza makala ya wilaya pia kigezo cha kata zake isipokuwa bado bila majina. Kata ya wilaya mpya bado zinaorodheshwa chini ya chini ya wilaya mama. Mifano ya wilaya mpya ni Wilaya ya Misenyi, Wilaya ya Chato, Wilaya ya Rorya.

Mikoa ya Tanzania ambayo kata zote zimeanzishwa makala ya mbegu[hariri chanzo]

Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kilimanjaro | Kigoma | Lindi | Mara | Mwanza | Mbeya | Manyara | Morogoro | Mtwara | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Mjini Magharibi | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini

Meta:List_of_Wikipedias_by_sample_of_articles inalinganisha wikipedia za lugha mbalimbali kwenye msingi wa orodha la Makala za msingi za kamusi elezo.

Katika ulinganisho wa Aprili 2009 makala zifuatazo ziliangaliwa hasa kuwa ama zinekosekana kabisa au ni fupi mno au ziko na ukubwa karibu na ngazi inayofuata (kati ya ndogo-wastani-kubwa na kila ngazi inapewa uzito tofauti katika ulinganisho).

Majina yafuatayo ni katika wikipedia ya Kiingereza.

  1. Song (wimbo - alama 463 pekee)
  2. Crusades - vita za misalaba
  3. Communism - ukomunisti
  4. Culture - utamaduni
  5. Bang Big Bang - mlipuko mkuu
  6. Evolution - mageuko ya spishi
  7. Democracy - demokrasia
  8. Horse - farasi
  9. Basketball - mpira wa kikapu
  10. Fashism - ufashisti

--Kipala (majadiliano) 17:21, 9 Aprili 2009 (UTC)[jibu]

Baada ya kutunga makala za mbegu kwa kila kata ya Tanzania tunalenga sasa kufanya kazi hiyohiyo kwa kata zote za Kenya. Ukurasa Wilaya, tarafa na kata za Kenya umeundwa kwa muda kwa kurahisisha utekelezaji wa mradi huu. Orodha hii inafikiwa pia kwa kifupikata Kenya.

Swahili Wikipedia now the largest African language Wikipedia[hariri chanzo]

Apologies for the English, I don't speak Swahili, but I thought I'd let everyone know that Swahili has just passed Afrikaans as the largest African language Wikipedia. Congratulations! See greenman.co.za for more information. Greenman (majadiliano) 22:12, 3 Agosti 2009 (UTC)[jibu]

It was time! - Don't you think so? - Congratulations!--Aristo Class (majadiliano) 13:48, 10 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

The Nairobi Hospital[hariri chanzo]

Apologies for the English, my Kiswahili are not that good. I've been writting an article (at the el:Wikipedia) about the "el:The Nairobi Hospital" and I do not have any pictures to support it. Can somebody from the Nairobi area, take several pictures of "The Nairobi Hospital" and upload them at Wikimedia Commons?
Asante sana!--Aristo Class (majadiliano) 20:58, 8 Septemba 2018 (UTC)[jibu]
P.S. I am particullarly interested of the "Galanos Block".
--Aristo Class (majadiliano) 16:05, 14 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Galanos sulphur baths[hariri chanzo]

Additive to The Nairobi Hospital request, I have another one, the following: I have written the el:Galanos sulphur baths at the Greek Wikipedia and do not have any pictures to accompany it. Can somebody from the el:Tanga Region, take several photographs of the "Galanos thermal springs" and upload them at Wikimedia Commons?
Asante sana!--Aristo Class (majadiliano) 16:01, 14 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Thanks for your contribution. We are a small group, at the moment I am not aware of anybody around Tanga. Lets see if we find someone. Kipala (majadiliano) 19:44, 19 Septemba 2018 (UTC)[jibu]
Dear Kipala, thank you very much for your response, I'll be waiting and hoping.
With kindest regards!--Aristo Class (majadiliano) 07:48, 22 Septemba 2018 (UTC)[jibu]


Afrocuration[hariri chanzo]

Hi all. I will be adding 4 articles relating to the Afrocuration project to add articles relating to Covid-19. Namely, Medical Diagnosis, Airborne Disease, Hand Washing, Environmental impact. Kind regards Dumbassman (majadiliano) 15:01, 6 Juni 2020 (UTC)[jibu]

@Riccardo Riccioni: can I upload the other 2 articles? Dumbassman (majadiliano) 16:17, 8 Juni 2020 (UTC)[jibu]
If you used computer translation, it's better if you don't upload them. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:51, 9 Juni 2020 (UTC)[jibu]
The 2 pages I created was made through an Afrocuration project done by translators that do speak Kiswahili and was not made through the content creation tool. Unfortunately I cannot gauge the quality of these articles. Were the other 2 of such poor quality that I shouldn't upload them? Thanks Dumbassman (majadiliano) 11:09, 9 Juni 2020 (UTC)[jibu]
Truly, the first one was very poor, the second one was a little better. Many times Swahili speakers are not so good translators! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:36, 9 Juni 2020 (UTC)[jibu]
Thanks a lot for your honest feedback. I will ask that the other 2 articles first be proofread. If anyone is keen to help the Google docs are available here and here. Thanks Dumbassman (majadiliano) 16:02, 9 Juni 2020 (UTC)[jibu]
Both articles need many corrections, though they are understandable. Let you upload them, then we will try to work on them. Thank you for your care and humble attitude. Peace to you! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:37, 10 Juni 2020 (UTC)[jibu]
Asante sana kwa maoni yako ya kweli. Nitauliza kwamba nakala zingine 2 kwanza zihakikiwe. Ikiwa mtu yeyote ana hamu ya kusaidia hati za Google zinapatikana hapa na

Dumbassman (majadiliano) 08:47, 13 Juni 2020 (UTC)[jibu]

Wikipedia pages Wanting Photos #WPWP[hariri chanzo]

Habari wachangiaji, katika mradi wa WPWP unaoendelea hivi sasa, kuna fujo nyingi za wachangiaji wakati wa kuongeza picha, kama kuacha maneno ya lugha nyingine katika maelezo juu ya picha. Hivyo ni ombi langu kwa wachangiaji angalau kupitia hizi makala na kufanya masahihisho. [kiungo hiki] Czeus25 Masele (majadiliano) 06:55, 10 Agosti 2020 (UTC)[jibu]

Ni kweli. Kwa tamaa ya tuzo wengine wanaongeza picha yoyote na maandishi yasiyo sahihi. Sisi hatuna muda wa kupitia kazi hizo zote. Hata hivyo kwa jumla faida fulani ipo. Amani kwenu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:01, 10 Agosti 2020 (UTC)[jibu]

Have you Voted?[hariri chanzo]

Hi all,

There are 16 eligible voters in Swahili Wikipedia for the ongoing Wikimedia Board of Trustees elections. But only one 3 people have voted so far.

The Wikimedia Foundation Board of Trustees election is still ongoing. Votes will be accepted until 23:59 31 August 2021 (UTC).

2021 Wikimedia Board election video:Please watch and share this widely so we can motivate more participation from all eligible voters!

Please visit here to cast your vote. You can also read more about the candidates here

Best, Zuz (WMF) (majadiliano) 10:07, 26 Agosti 2021 (UTC)[jibu]

2021 Wikimedia Board of Trustees Election Result[hariri chanzo]

Thank you to everyone who participated in the 2021 Board election. The Elections Committee has reviewed the votes of the 2021 Wikimedia Foundation Board of Trustees election, organized to select four new trustees. A record 6,873 people from across 214 projects cast their valid votes. The following four candidates received the most support:

While these candidates have been ranked through the community vote, they are not yet appointed to the Board of Trustees. They still need to pass a successful background check and meet the qualifications outlined in the Bylaws. The Board has set a tentative date to appoint new trustees at the end of this month.

Read the full announcement here. Best, Zuz (WMF) (majadiliano) 10:49, 8 Septemba 2021 (UTC)[jibu]


Campaigns Ambassador Contractor Opening For African French, Arabic And Swahili Speakers[hariri chanzo]

Dear Swahili Wikipedia Community,

The Campaigns Team at the Wikimedia Foundation is excited to announce that it seeks a Campaigns Ambassador with experience working in the French, Arabic or Swahili Wikipedia communities in Africa.

The campaign ambassador will support our product and programs team in providing support and advising to campaign organizers and improve the campaign organizing journey. The Campaigns Ambassador will be supporting the rollout of tools and features to support campaign organizers, in the communities we are building for.

Kindly confirm further details and requirements about the role in the attached job description. All interested applicants should submit a copy of their curriculum vitae (CV) and cover letter via email to fnartey@Wikimedia.org and copy ifried@wikimedia.org by 28th November 2021.

If you have any further questions about the role kindly contact jjonsson@wikimedia.org.

Thank you.

Best,
Imelda

Voting closes soon on the revised Enforcement Guidelines for the Universal Code of Conduct[hariri chanzo]

You can find this message translated into additional languages on Meta-wiki.
More languages Please help translate to your language

Hello all,

Voting closes on the revised Universal Code of Conduct Enforcement Guidelines at 23.59 UTC today, January 31, 2023. Please visit the voter information page on Meta-wiki for voter eligibility information and details on how to vote. More information on the Enforcement Guidelines and the voting process is available in this previous message.

On behalf of the UCoC Project Team,

Zuz (WMF) (majadiliano) 10:14, 31 Januari 2023 (UTC)[jibu]