Majadiliano ya mtumiaji:Baba Tabita
| Mtumiaji huyu ana kazi nyingi katika maisha ya kweli na hawezi kujibu maswali yako kwa uharaka zaidi. |
Majadiliano ya zamani yanaonekana kulingana na miaka:
| Archives |
|---|
Mpmayenge
Salamu BT,naomba unisaidie kubatilisha jina langu la matumizi hapa. Ahsante Limoke oscar (majadiliano) 12:31, 19 Aprili 2011 (UTC)
Photo request
Where would I place a photo request?
I would like for someone to photograph the Kenya Airways head office on Airport Road North in Embakasi, Nairobi.
Thanks WhisperToMe (majadiliano) 22:23, 4 Desemba 2010 (UTC)
- Thank you! I'll ask Abbas WhisperToMe (majadiliano) 02:21, 30 Desemba 2010 (UTC)
- Hi again. Abbas hasn't edited since December. I do not know where the Wikimedia Kenya member list is. Where may I see the list? Thank you, WhisperToMe (majadiliano) 21:10, 6 Februari 2011 (UTC)
- Try wikimedia.or.ke - his email is listed there as contact person. --Baba Tabita (majadiliano) 03:11, 7 Februari 2011 (UTC)
- Thank you very much! WhisperToMe (majadiliano) 01:59, 8 Februari 2011 (UTC)
- I sent Abbas the e-mail explaining the two requests at JKIA Airport WhisperToMe (majadiliano) 02:04, 8 Februari 2011 (UTC)
Karibu / Welcome
Tumejadiliana na Muddy kuhusu kile Kigezo cha Karibu / Welcome. Nimebadilisha "Karibu" kwa kuongeza sentensi ya Kiingereza. Machoni pangu inatosha. Wakati wanapojiandikisha si rahisi kuona kwa kila mtu kama anajua au hajui Kiswahili (asipoweka ile Babel-sw 0 mwenyewe). Kwa hiyo nadhani maelezo mengi si lazima maana hao wanahitaji kufika ama ukurasa wa Bots au kufika kwa wakabidhi. Machoni pangu si lazima kutumia kile cha kiingereza pekee. Unaonaje? Kipala (majadiliano) 14:48, 9 Desemba 2010 (UTC)
- Sawa, nakubali. Sitaitumia tena. Asante kwa rekebisho hilo. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 09:31, 23 Desemba 2010 (UTC)
Please, could you translate en:Podolsk into Kiswahili? Naturally if you have available time!
Good day to you! Could you, please, translate into Kiswahili the article, containing two-three sentences, about this city in Russia? I’d like to thank you in advance :)--Переход Артур (majadiliano) 10:53, 15 Februari 2011 (UTC)
Viungo vya mwili
Oliver, salaam. Nina ombi. Niliwahi kuanzisha makala juu ya viungo vya mwili na hao vijana wa mashindano ya makala za afya waliendelea. Makala hizi zote zinahitaji kuangaliwa kwa sababu Wakenya (nadhani) waliunda sentensi za ajabu kidogo na pia mara kadhaa walikosa viungo. Nikiingia hapa naona udhaifu: kwa Wasafwa na Wanyakyusa nilipojifunza Kiswahili na baadaye Nairobi sijasikia kitu kingine ila "mkono" na "mguu". Kumbe. Sasa nimetengeneza picha ya mkono nikilenga kutaja sehemu zake kuanzia bega kupitia kisugidi hadi kiganja. Lakini ninahisi ya kwamba sina uhakika kwa sababu sina uzoefu kutaja sehemu zile (yooote mkono!) na kamusi zangu si wazi sana; mara nyingi maelezo si kamili, yanaingiliana maana au kuna maneno kadhaa na mimi sijui lipi ni afadhali. Je unajua wewe majina haya au unaweza kuchungulia kidogo? Tuanze kumaliza mkono baadaye inafuata mguu na mengine! (the hand was cut from the arm tusemeje?? foot from the leg?? ) Kipala (majadiliano) 20:56, 10 Aprili 2011 (UTC)
- Asante kwa ombi, mzee wangu. Umenipa kitendawili kwelikweli. Sina uhakika kama nitapata majibu. Usipopokea ujumbe kutoka kwangu naomba unikumbushe tena. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 06:25, 11 Aprili 2011 (UTC)
Ombi
Muddy, Oliver salaam! Najua mna kazi nyingi siku hizi poleni lakini naomba ushauri wenu kuhusu mchangiaji mgeni Mjanja. Naona si msemaji wa lugha hadi sasa anaandika makala mbegu na anajadiliana kwa Kiingereza tu. Ameingia kwa mbio pia naona ana uwezo wa kujifunza haraka kwa hiyo akibaki anaweza kuendelea kuwa mwenzetu anayesaidia kujenga sw. Kwa upande mwingine ameonyesha tabia kadhaa kama vile kubadilisha makala bila maelezo n.k. ambayo labda ni shauri la kuwa mgeni. Sasa ameanza kwa mbio kubadilisha majina ya makala na kuhamisha makala na inahusu makala nilizoanzisha mimi ni afadhali kiutaratibu kama mmoja wenu anaweza kuangalia mambo. Alianza na majina ya nchi - hapa ni wazi tunahitaji majadiliano ya kuendelea. Ameendelea kwa majina ya sayari hadi kuleta mashtaki Majadiliano:Utaridi nikimjibu itaelekea upande ambao hadi sasa hatujakuwa nao yaani "vita ya uhariri". Habari za fujo la majina ya sayari zilijadiliwa miaka kadhaa iliyopita haleti kitu kipya. Sidhani ya kwamba anaelewa chote nilichomwandikia kwa Kiswahili. Picha yangu ni anakaa mbele ya kamusi zake sijui wapi na hapa anaona nuru basi penginepo giza. Sitaki kupoteza muda kuvutana juu ya hayo lakini pia si sawa kumwacha mgeni aliyefika juzi tu (bila uwezo wa kuandika sentensi 3,4 za Kiswahili -hadi sasa) kukoroga makala. Kipala (majadiliano) 10:47, 23 Aprili 2011 (UTC)
Article requests
Where do I put article requests?
I would like to request en:Mohamed Amin - He was a well known Kenyan photojournalist who worked in Ethiopia. en:Ethiopian Airlines Flight 961 would also be a good one to request (the plane was supposed to land in Kenya) WhisperToMe (majadiliano) 11:49, 8 Mei 2011 (UTC)
- Don't think we have a page for article requests. Sorry! Guess you best keep suggesting it on individual's talk pages (try some of the recently active Kenyan students). Sorry again not to be of better help right now. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 18:42, 10 Mei 2011 (UTC)
- Thank you :) WhisperToMe (majadiliano) 10:52, 11 Mei 2011 (UTC)
- Hi, sorry I don't know your name, but thanks for your concern on the articles request. I am currently held up in school but I will find time to translate the articles you requested for. Regards Coolsam726 (majadiliano) 00:49, 4 Juni 2011 (UTC)
- Thank you :) WhisperToMe (majadiliano) 10:52, 11 Mei 2011 (UTC)
Mohamed ElGedawy → محمد الجداوي
Hi, I want to change my name from: "Mohamed ElGedawy" to: "محمد الجداوي", Because i have changed my username on many wikipedias.--Mohamed ElGedawy (majadiliano) 07:42, 14 Agosti 2011 (UTC)
- Imefanyika. / Done. --Baba Tabita (majadiliano) 12:14, 14 Agosti 2011 (UTC)
GedawyBot
Hi sir. I made a request for bot flag here.--محمد الجداوي (majadiliano) 15:06, 28 Agosti 2011 (UTC)
Imefanyika. --Baba Tabita (majadiliano) 18:12, 28 Agosti 2011 (UTC)
Hongera ya mbegu za lugha!
Salaam, Oliver! Eh, nimependa zile mbegu za lugha ulizopanda! Mwongozo na hamasa njema kwa sisi tuliokimbia.. Labda uwe mfano wa kuigwa! Shukrani sana.--MwanaharakatiLonga 06:06, 24 Oktoba 2011 (UTC)
- Asante sana tena sana kwa kunihamasisha. Pamoja tusonge mbele! --Baba Tabita (majadiliano) 07:01, 24 Oktoba 2011 (UTC)
-
- BT, salam. Eti hizi mbegu za lugha unatumia msaada wa mashine, yaani, Auto-Wiki-Browser au unafanya moja-moja?--MwanaharakatiLonga 14:36, 27 Oktoba 2011 (UTC)
- Salaam nawe, Muddyb. Naziandika mojamoja usiku katika Word wakati wa ukosefu wa mtandao halafu nazipakua nitakapoingia ofisini tena asubuhi yake. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 05:13, 28 Oktoba 2011 (UTC)
Basi elewa nimeipenda! Namba zimekuwa kubwa kwelikweli. Hongera tena!--MwanaharakatiLonga 06:05, 28 Oktoba 2011 (UTC)
Lugha za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Pole na kazi kubwa! Naomba uangalie pia makala Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na jinsi lugha zinavyotajwa humo. Nimeshaweka redirect kwa Kikongo maana inaonekana ni umbo lingine la kuiandika, halafu ile Kitshiluba / Tshiluba sijaona kwako labda Kiluba? Kipala (majadiliano) 12:00, 28 Oktoba 2011 (UTC)
- Asante kwa pole yako. Kweli, nimeuangalia ukurasa wa nchi yenyewe (ndipo nilipoanza kwa kuweka kiungo cha orodha ya lugha). Ukiangalia katika tovuti ya Ethnologue kwa DRC utaona kuwa kuna tofauti kati ya Kikongo ambacho ni kundi la lugha mbalimbali zisizoeleweka moja kwa nyingine na Kikoongo ambacho ni lugha mojawapo ya lugha za kundi hilo. Sawa? Pia kwa kawaida nimetumia kiambishi cha Kiswahili kwa lugha, yaani Ki-, kwa kila lugha. Upande wa Kiluba (kwa Kiingereza "Luba language") naona tutumie Ki- badala ya Tshi-, maana yake Kiluba ni Kiswahili na Tshiluba ni jina la lugha katika lugha yenyewe. Halafu kusema Kitshiluba ingekuwa kama kusema kwa Kiingereza "the Kiswahili language". Haya, mzee wangu, asante kwa kushauriana. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 12:14, 28 Oktoba 2011 (UTC)
- BAsi naomba usahihishe pia lugha katika makala yenyewe, maana sijui kuchagua Kiluba ipi (ziko mbili nisipokosei?). Ila tu kuhusu Kikoongo / Kikongo nasoma ethnologue tofauti kidogo. Hapa naona "Kikongo" ni jina badala katika Kongo na pia jina la lugha katika Angola. Amua wewe lakini naona mahali pengine wengi wataona jina "Kikongo" maana nisipokosei ni umbo la kawaida kwa Kiingereza (nimeona Koongo mara ya kwanza leo - asanten kwa elimu!) Kipala (majadiliano) 17:08, 28 Oktoba 2011 (UTC)
- Samahani, mzee wangu. Sijaelewa unamaanisha nini ukiniomba kusahihisha lugha katika makala. Kweli kuna lugha nyingi za Kiluba; hata wikipedia ya Kiingereza inaeleza hivi hapa. Pia inatofautisha Kiluba-Kasai na Kiluba-Katanga nilivyofanya na mimi katika makala za Kiluba. Kuhusu Kikongo, nimefuata ukurasa huu; kwa hiyo Kikongo kinachozungumzwa nchini Angola ni Kikongo cha San Salvador au Kisikongo lakini lugha ya kitaifa nchini DRC ni Kikoongo. Kweli, bado "redirect" nyingi zinahitajika. Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 06:47, 31 Oktoba 2011 (UTC)
Great work!
Salaam, mbona unazidi kunishangaza tu? Sasa unatisha bwana mkubwa! Nimeona ukipanda mbegu kwa kasi ya ajabu, haijakutosheleza: umeamua kuongeza viungo vya nje kadhaa kwa kutumia programu ya nusu-auto ili ufanikishe zoezi kwa uharaka zaidi. Nimeipenda Oli! Tusonge zaidi, BT!--MwanaharakatiLonga 05:28, 12 Desemba 2011 (UTC)
- Asante kwa pongezi lako! Ndiyo shabaha yangu kuharakisha kazi - Waswahili wengi zaidi wataingia mtandaoni hivi karibuni. Tuwe tayari! Tena, naona umuhimu wa kuanzisha makala zihusuzo mada za Kiafrika kama vile za lugha za Kiafrika au waandishi Waafrika. Haya, kweli, tusonge mbele! Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 06:07, 12 Desemba 2011 (UTC)
-
- Mh, ninawasubiria kwa hamu! Wache waje - angalau tuwe wengi na tuboreshe wikipedia yetu! Tupo kwa ajili yao...--MwanaharakatiLonga 06:53, 12 Desemba 2011 (UTC)
Makala za Wabunge wa Tanzania
NAona siku hizi umefika tena kwa nguvu. Kuhusu makala za wabunge: kwa bahati mbaya hakuna miaka ya huduma inayotajwa.NAdhani bunge mpya inakaribia na baadaye itakuwa kazi ya kuangalia upya maana wengine waliowekwa sasa hawatarudi. Ningependelea kama sentensi inaweza kuingizwa inayotaja muda wa huduma kwa sasa. Labda yuko anayeweza kutunga programu inayoandika haya? Kipala (majadiliano) 15:58, 19 Desemba 2011 (UTC)
- Asante, mzee wangu. Kweli, nimejaribu kurahisisha kuingiza miaka ya ubunge kupitia kwa AWB lakini siyo rahisi nilivyofikiri kwanza. Hata kupata habari kuhusu wabunge ni kazi. Nitaitafakaria tena ... Univumilie! Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 05:34, 20 Desemba 2011 (UTC)
- Inaonekana ni lazima kutumia tovuti rasmi ya Bunge la Tanzania. Sasa, sioni njia kuingiza habari hizo automatically :( - au una wazo lingine? Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 10:28, 20 Desemba 2011 (UTC)
Mafuriko Tanzania Jamani eeeh!!!!!
Oliver salam, wenzenu huku mjini Dar es Salaam na baadhi ya mikoa ya Tanzania tuna hali mbaya vibaya mno. Kuna mvua inaendelea kunyesha kwa kasi ya ajabu na mafuriko hadi sasa yauwa na kuharibu majumba kibao hakuna mfano. Chakusikitisha, bado haijasimama. Inaendelea kuleta ladha ya vifo kwa wakazi wa Tanzania. Mtuombeee huko!!!! Wenu!--MwanaharakatiLonga 06:05, 22 Desemba 2011 (UTC)
- Asante kwa kutujulisha! Tunawaombeeni! Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 08:11, 22 Desemba 2011 (UTC)
Swali moko!
Salaam, eti Oliver wewe binafsi ni sawa kuweka mabano katika kila makala utakayoianzisha kuhusu malugha? Wakati mwingi nimekuwa nikikuta makala moko (moko= moja) tu halafu ina-mabano! Yaani hivi, hakuna makala nyingine zaidi ya ile yenye mabano! Pwaaa!--MwanaharakatiLonga 16:39, 22 Desemba 2011 (UTC)
- Asante kwa swali zuri. Nitajitahidi kuweka 'redirect' pia. Nimeona vema wasomaji waelewe moja kwa moja kwamba ni lugha (mara nyingi kuna kata au wilaya yenye jina lilelile). Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 17:02, 22 Desemba 2011 (UTC)
- Hapo chacha nimeelewa! Shukrani kwa jibu la haraka zaidi!--MwanaharakatiLonga 17:17, 22 Desemba 2011 (UTC)
- Ndugu Muddyb, sasa tu nimeona kuwa katika wikipedia ya Kiingereza wanakataa mabano yasiyo lazima. Ndiyo sababu nimeanza kuyaondoa tena. Ila nimeanza pia kuweka 'redirect'. Haya, tusonge mbele! Wasalaam, --Baba Tabita (majadiliano) 18:54, 8 Januari 2012 (UTC)
-
- Salaam, BT. Nimekufagilia mtu wangu kwenye blogu yangu!--MwanaharakatiLonga 10:45, 23 Desemba 2011 (UTC)