Italia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
|
|
|||
| Lugha rasmi | Kiitalia; kijimbo pia Kijerumani, Kifaransa, Kiladino, Kislovenia, Kisardinia | ||
| Mji Mkuu | Roma | ||
| Rais | Giorgio Napolitano | ||
| Waziri Mkuu | Silvio Berlusconi | ||
| Eneo | 301.338 km² | ||
| Wakazi | 59,905,225 (2008) | ||
| Wakazi kwa km² | 198.8 | ||
| JPT | 31,022 US-$ (2008) | ||
| Pesa | Euro | ||
| Wakati | UTC+1 | ||
| Wimbo la Taifa | Fratelli d'Italia (Ndugu Waitalia) | ||
| Sikukuu ya Jamhuri | 2. Juni | ||
| Sikukuu ya Taifa | 25. Aprili | ||
| Simu ya kimataifa | +39 | ||
Jamhuri ya Italia ni nchi ya Ulaya Kusini. Eneo lake ni 301.338 km² ambalo lina wakazi 59,905,225 (2008).
Umbo lake linafanana na mguu linalozungukwa na maji ya Mediteraneo pande tatu. Visiwa viwili vikubwa vya Sicilia na Sardinia ni sehemu za Italia pamoja na visiwa vidogovidogo.
Imepakana na Ufaransa, Uswisi, Austria na Slovenia.
Nchi mbili ndogo zinazozungukwa na eneo la Italia ni San Marino na Vatikano.
Peninsula hiyo iliunganishwa mara ya kwanza na Jamhuri ya Roma (509-27 K.K.), lakini hiyo ilipoenea Ulaya, Afrika ya Kaskazini na Asia ya Magharibi ikawa na sura ya kimataifa.
Umoja ulipotea kuanzia uvamizi wa Roma (476) na hasa baada ya ufalme wa Karolo Mkuu.
Juhudi za kuurudisha zilifanywa hasa katika karne ya 19, ambapo Ufalme wa Sardinia ulitekwa sehemu kubwa ya Italia (hasa miaka 1860, 1866 na 1870).
Baada ya vita vikuu vya pili iligeuka Jamhuri yenye katiba inayotia mamlaka kuu mikononi mwa bunge.
Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957 ikaendelea kuunga mkono ustawi wake hadi uanzishaji wa pesa la pamoja (Euro).
Italia ni nchi iliyoendelea, ikiwa na nafasi ya sita kwa nguvu ya kiuchumi duniani, hivyo ni mwanachama wa G7 na G8.
Pia ni nchi inayongoza duniani kwa kuwa na mahali pengi (40) pa kihistoria palipoingizwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".
[hariri] Tazama pia
| Nchi za Umoja wa Ulaya | |
|---|---|
| Austria | Bulgaria | Cyprus | Denmark | Estonia | Finland | Hungaria | Ireland | Italia | Latvia | Lithuania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Hispania | Romania | Sweden | Ubelgiji | Uceki | Ufaransa | Ugiriki | Uholanzi | Uingereza| Ujerumani | Ureno | |
| Makala hii kuhusu maeneo ya Italia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Italia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |