Leonardo da Vinci
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Leonardo da Vinci (15 Aprili, 1452 – 2 Mei, 1519) alikuwa ni mchoraji mahiri Muitalia, pia alikuwa ni Mwanafalsafa, Mwanamahesabu na Injinia Mchora ramani za majengo.
[hariri] Maisha ya Mwanzo
Familia ya Leonardo iliishi Anchiano toka karne ya 13. Leonardo alizaliwa tarehe 15 Aprili, 1452 kwenye nyumba ya mkulima mahali panapoitwa Anchiano, yapata kilometa 3 kutoka Vinci Italia. Jina lake la kubatizwa ni Lionardo na siyo Leonardo. Baba yake Leonardo aliitwa Ser Piero, na mama yake aliitwa Catarina. Mwaka alipozaliwa Leonardo, baba yake alikuwa na umri wa miaka 25 na katika mwaka huohuo alimwoa mwanamke mwingine ambaye alikuwa ni mke wake wa kwanza aliyeitwa Albiera, hakumwoa mama yake Leonardo, sababu mama yake Leonardo alikuwa ni mwana wa mkulima na alitoka katika familia duni, hiyo ilitokana na ubaguzi wa matabaka kwa wakati huo. Leonardo aliishi Anchiano kwa kipindi cha miaka 5 tu toka alivyozaliwa, na mwaka 1457 aliondoka Achiano alipokuwa akiishi na babu yake na kwenda mji wa Vinci, na kuanzia hapo akawa ni mwanafamilia wa baba yake. Ser Piero na mke wake hawakufanikiwa kupata mtoto, na pengine hiyo ilikuwa ni sababu ya Leonardo kuwa mwanafamilia wa baba yake.
Mwaka 1466 aliondoka Vinci na kwenda mji wa Florence. Leonardo alianza kutambulika kutokana na uchanganyaji wake wa rangi katika michoro yake. Wakati alipokuwa kwenye makongamano ya sanaa - hii ilikuwa ni kati ya miaka ya 1466 na 1472 -, michoro yake ilikuwa bado haijatambulika, lakini Leonardo alikazana na kuanza kuchora kwa bidii huku akitumia rangi za mafuta na zoezi hilo alipewa na msanii MDachi. Mwezi wa Juni 1472, Leonardo aliorodheshwa katika kitabu chekundu cha wachoraji wa Florence kilichoitwa: Campagnia de pittori. Pia alipewa uanachama wa wachoraji wa Florence.
[hariri] Kifo
Mwaka 1516 Leonardo alikwenda Amboise, Ufaransa, baada ya kupata mualiko kutoka kwa mfalme Francis wa kwanza na kati ya mizigo aliyosafiri nayo ulikuwemo mchoro maarufu wa Monalisa. Leonardo aliishi Amboise toka mwaka huo wa 1516 mpaka mwaka 1519, alifariki Mei 2 1519 mjini Amboise na kuzikwa St. Hubert akiwa na umri wa miaka 67, lakini taarifa za afya yake hazikuwa nzuri kwasababu Leonardo alipata ugonjwa wa kiharusi toka mwaka 1517 lakini taarifa za ugonjwa wake zikatolewa wiki chache kabla ya kifo chake.
| Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Leonardo da Vinci kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |