Hadithi
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hadithi ni sehemu ya fasihi. Hasa kuna aina mbili za hadithi:
- hadithi za kubuni,
- hadithi za kihistoria.
Hadithi za kubuni [hariri]
- Ngano za mazimwi: Wahusika wakuu huwa mazimwi ambao hupewa sifa zinzowatenga na binadamu wengine wa kawaida.
- Ngano za mashujaa: Husimulia visa na vitendo na matukio ya kishujaa yanayohuhusiana na shujaa wa jamii fulani.
- Ngano za usuli: Hutoa asili au chanzo cha jambo.
- Hekaya: Hizi ni hadithi za kijanja...mhusika mmoja rafiki wa wengine hupitia njia ya ila na ujanja.
- Ghurufa: Wahusika huwa wanyama waliowakilisha wanadamu wenye sifa za wanadamu hao.
- Ngano za kimafumbo: Huwa na mafumbo yenye maana nyingine ya ndani.