Neno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Neno ni sehemu fupi ya lugha yenye maana. Ni sauti inayotamkwa au kuandikwa pamoja na kutaja jambo fulani.

Neno linaweza kuwa fupi lenye mofimu (yaani sauti inayowakilisha maana fulani) moja tu au kuwa ndefu lenye mofimu mbalimbali.

Wataalamu wanaona neno ni sehemu ya lugha yenye kituo kidogo mbele na nyuma yake, au kwa maandishi jumla ya herufi zenye maana zilizotengwa kwa nafasi nyuma na mbele.

Katika mazungumzo wakati mwingine si rahisi kutofautisha maneno kama ni maneno marefu au maneno mawili. Kwa mfano kuna maneno yaliyobuniwa juzi tu kwa kutaja mambo ya teknolojia na sayansi ambayo yanaunganisha maneno mawili kuwa moja:

  • garimoshi (gari + moshi) kama kifupi cha "gari la moshi" iliyokuwa kawaida zamani
  • mawasilianoanga (mawasiliano + anga - "telecommunication")

Si wazi mara moja kwa wakilizaji wanaosikia haya mara ya kwanza kama ni neno moja au maneno mawili.

Wataalamu wa lugha hutofautiana aina za maneno kama vile nomino, kitenzi, kivumvishi, kielezi, kiunganishi na vingine.

Maneno kwa pamoja yanaunda sentensi yakifuata masharti ya sarufi katika lugha.


Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.