Treni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Treni za TRC kituoni huko Dar es Salaam.
Treni.

Treni (kutoka Kiingereza train; huitwa pia gari la moshi au garimoshi) ni chombo cha usafiri kwenye reli za garimoshi. Pia anaendesha hili jombo anaitwa nahodha.

Treni inamaanisha jumla ya mabehewa inayovutwa au kusukumwa na injinitreni kwenye njia ya reli. Mfumo wa usafiri kwa treni huitwa kwa kifupi reli.

Mabehewa haya yanaweza kubeba watu au mizigo, hivyo kuna tofauti kati ya treni ya abiria na treni ya mizigo.

Mahali ambako treni inasimama na kupokea abiria au mizigo huitwa kituo cha reli.

Picha

Treni