Usafiri
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Treni ya Shinkansen nchini Japani
Feri kwenye bandari ya Dar es Salaam
Ndege ya Boeing 747-300
Usafiri ni uhamisho wa watu au vitu na bidhaa kutoka mahali pamoja kwenda mahali pengine.
Usafiri unakuja pamoja na muundombinu kama njia za usafiri, vyombo vya usafiri na wahusika wake kama makampuni, shirika na abiria.
Njia za Usafiri [hariri]
Njia za usafiri hutofautishwa kufuatana na aina yake kama ni
- usafiri wa nchini kwa kutumia barabara au reli
- usafiri wa majini kwa kutumia bahari, maziwa, mito na mifereji
- usafiri wa hewani kwa kutumia vyomboanga na viwanja vya ndege
Vyombo vya usafiri [hariri]
Vyombo vya usafiri hulingana na njia zinazotumia.
Usafiri wa nchini hutumia motokaa, treni, baisikeli au pikipiki.
Usafiri wa majini hutumia meli, boti, jahazi na mengine