Dar es Salaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Dar es Salaam
Mjini Dar es Salaam inavyoonekana kutoka Mafuta House
Mjini Dar es Salaam inavyoonekana kutoka Mafuta House

Nembo
Dar es Salaam is located in Tanzania
Dar es Salaam
Dar es Salaam
Lokeshen Dar es Salaam
Anwani ya kijiografia: 6°48′S 39°17′E / 6.8°S 39.283°E / -6.8; 39.283
Nchi Tanzania
Mkoa Dar es Salaam
Idadi ya wakazi (2002)
 - Mji 2,497,940

Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania. Ni pia jina la Mkoa wa Dar es Salaam. Hali halisi ni pia mji mkuu wa Tanzania hata kama Dodoma imetangazwa kuwa mji mkuu tangu mwaka 1973. Lakini ofisi ya rais na wizara nyingi bado zinafanya kazi Dar es Salaam ambayo hali halisi ni makao makuu ya serikali.

Yaliyomo

[hariri] Historia

Jiji hili zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotoka kwenye Kiarabu دار السلام (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).

Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia kwenye mdomo pana ya mto Kurasini. Kuanzia 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala. Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu 1904 ziliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara kuwa koloni ya Tanganyika chini ya Uingereza.

[hariri] Wakazi na uchumi

Dar es Salaam inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao milioni tatu. Ingawa Dodoma inafahamika kama ndio mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam ndiko ziliko ofisi kuu za viongozi wa serikali, mabalozi, mashirika ya kimataifa, n.k.

Uwanja wa ndege mkuu wa Tanzania uko pia mjini hii ni Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere. Bandari ya Dar es Salaam katika bahari ya Hindi, ndio bandari kubwa nchini Tanzania inayojihusisha na usafirishaji na uingizaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, ujenzi, magari, madawa, n.k.

Kiutawala, Dar es Salaam imegawanywa katika wilaya za Temeke, Ilala, na Kinondoni.

[hariri] Viungo vya nje

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

[hariri] Picha za Dar es Salaam

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine