Jiji
Jiji ni mji mkubwa. Kuna tofauti kati ya nchi na nchi ni sifa gani pamoja na ukubwa gani zinazofanya mji kuwa mji mkubwa au jiji.
Yaliyomo |
Majiji ya Afrika ya Mashariki[hariri]
Nchini Tanzania ni Dar es Salaam pamoja na Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga, inayoitwa "jiji"; nchini Kenya ni Nairobi pamoja na Mombasa na Kisumu. Kati ya hii ni Nairobi na Dar es Salaam pekee yenye wakazi zaidi ya milioni moja.
Mji mkubwa kwa kanuni za takwimu[hariri]
Kimataifa kulikuwa na makubaliano kwenye mkutano wa kimataifa ya takwimu ya mwaka 1887 ya kuhesabu kila mji mwenye wakazi zaidi ya 100,000 kama "mji mkubwa", miji kati ya wakazi 20,000 na 100,000 kama miji ya wastani na miji kati ya wakazi 5,000 na 20,000 kama miji midogo. Kufuatana na hesabu hii kulikuwa na miji mikubwa 1,700 duniani wakati wa mwaka 2002.
Mfano wa China[hariri]
Nchi ya China pekee yake ina miji mikubwa 668. Penye wakazi 100,000 - 200,000 huitwa jiji dogo nchini China, kati ya wakazi 200,000 - 500,000 ni jiji la wastani, 500,000 hadi milioni 1 ni jiji kubwa. Penye wakazi wanaozidi milioni 1 huitwa jiji kubwa sana.
Jiji na City[hariri]
Jiji hutafsiriwa mara nyingi kwa neno "city" kwenye lugha ya Kiingereza lakini "city" haina sifa maalumu zinazokubaliwa katika Uingereza au Marekani. Kuna miji midogo inayoitwa "City" pia.
Majiji makubwa ya dunia[hariri]
Leo hii kuna majiji 20 yenye wakazi zaidi ya milioni 10:
- Tokyo, Japani - miloni 28
- Mexico City, Mexico - miloni 18
- Mumbai, Uhindi - miloni 18
- São Paulo, Brazil - miloni 18
- New York City, Marekani - miloni 17
- Shanghai, China - miloni 14
- Lagos, Nigeria - miloni 13
- Los Angeles, USA - miloni 13
- Kalkutta, Uhindi - miloni 13
- Buenos Aires, Argentina - miloni 12
- Seoul, Korea ya Kusini - miloni 12
- Beijing, China - miloni 12
- Karachi, Pakistan - miloni 11
- New Delhi, Uhindi - miloni 11
- Dhaka, Bangladesh - miloni 11
- Manila, Ufilipino - miloni 11
- Cairo, Misri - miloni 11
- Osaka, Japani - miloni 11
- Rio de Janeiro, Brazil - miloni 11
- Tianjin, China - miloni 10
- Johannesburg, RSA - miloni 7