Aleksandria
| Aleksandria | |
| Mwambao wa Mediteranea huko Aleksandria | |
| Mahali pa mji wa Aleksandria katika Misri | |
| Anwani ya kijiografia: 31°12′N 29°55′E / 31.2°N 29.917°E | |
| Nchi | Misri |
|---|---|
| Mkoa | Aleksandria |
| Idadi ya wakazi (2006) | |
| - Mji | 4,110,015 |
Aleksandria (pia: Alexandria; Kigiriki Ἀλεξάνδρεια Alexandreia; Kiarabu: الإسكندرية al-iskandariya) ni mji mkubwa wa pili wa Misri na bandari muhimu kwenye Bahari ya Mediteranea.
Iko kando la delta ya Nile kwenye kaskazini ya Misri takriban 225 km kutoka Kairo.
Jina la mji limetokana na mfalme Aleksander Mkuu wa Makedonia ya Kale aliyeunda mji mwaka 331 KK.
Waptolemaio waliotawala Misri baada ya Aleksander waliifanya kuwa mji mkuu wa milki yao na kitovu cha elimu na sayansi. Maktaba ya Aleksandria yalikuwa na vitabu vingi kushinda maktaba zote za dunia na wataalamu kutoka nchi nyingi walikuja hapa kwa masomo yao. Pharos ya Aleksandria ilikuwa mnara wa taa iliyohesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia ya kale.
Mji ulistawi hadi uenezaji wa Waislamu waliounda mji mkuu mpya huko Kairo.
Baadaye Aleksandria ilibaki kama mji muhimu wa uchumi na biashara wa Misri na bandari kuu ya nchi hadi leo.
Viungo vya nje [hariri]
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Aleksandria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |