Maajabu ya dunia
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Maajabu saba ya dunia)
Maajabu ya dunia ilikuwa orodha ya majengo saba ya pekee iliyojulikana kwa Wagiriki wa kale.
Mara ya kwanza majengo haya yalitajwa na mwandishi Herodoti (mnamo 450 KK). Wagiriki waliita majengo haya ΤÀ ΕΠΤÀ ΘΕÁΜΑΤΑ ΤΗΣ ΟΙΚΟΥΜÉΝΗΣ (ΓΗΣ) ta hepta theamata tes oikumenes (ges) - Maajabu saba ya dunia inayokaliwa).
[hariri] Maajabu saba ya Kale
- Piramidi za Giza (Misri ya Kale)
- Mabustani ya Semiramis (Babeli)
- Hekalu ya Artemis mjini Efeso (Asia Ndogo)
- Sanamu ya Zeus mjini Olympia (Ugiriki ya Kale)
- Kaburi la Mausolo mjini Halicarnasso (Uajemi)
- Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos (Ugiriki ya Kale)
- Mnara wa Pharos ya Aleksandria (Misri)
Piramidi pekee zimebaki hadi leo.

