Kitabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vitabu

Kitabu (Kar. كتاب kitabun) ni mkusanyo wa kurasa zilizofungwa pamoja kwa njia ya kudumu. Siku hizi kitabu kimekuwa hasa mkusanyo wa kurasa za karatasi zilizochapishwa. UNESCO imetoa elezo kuwa kitabu ni tangazo kwa umma lililochapishwa lenye kurasa zisizopungua 49.

Lakini kuna pia vitabu vyenye kurasa tupu vitakavyoandikiwa kwa mkono. Hadi karne ya 15 BK vitabu vyote viliandikwa kwa mkono kwa kutumia kalamu na kwa sababu hii vilikuwa vichache na bei ilikuwa juu. Johannes Gutenberg alibuni mashine ya kuchapisha vitabu iliyofaulu na kurahisisha vitabu sana.

Siku hizi vitabu hutolewa pia kwa njia ya mtandao au CD kama vitabu pepe.

Kitabu kilichochapishwa mara nyingi duniani ni Biblia ya Kikristo imetolewa kwa nakala bilioni 5-6.


[hariri] Viungo vya Nje


WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Kitabu" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Kitabu kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.