Bara Hindi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bara Hindi
Bara Hindi inavyoonekana kutoka angani.

Bara Hindi (Kiing. Indian subcontinent) ni eneo kubwa la Asia kusini kwa milima ya Himalaya lenye kilomita za mraba milioni 4.5. Eneo hili huitwa pia mara nyingi "Asia ya Kusini".

Inaingia ndani ya bahari Hindi kama rasi kubwa sana lenye umbo la pembetatu.

Nchi za Bara Hindi

Nchi zifuatazo ni sehemu za Bara Hindi:

Pia kuna nchi zifuatazo katika visiwa vya jirani:

Jiografia

Kijiografia kuna sehemu tatu:

  • maeneo ya Himalaya (kaskazini mwa Uhindi na mwa Pakistan, Nepal, Bhutan)
  • rasi ya Uhindi
  • maeneo ya visiwa vya Bahari Hindi (Sri Lanka, Maldivi)

Kijiolojia Bara Hindi si sehemu ya Asia. Inakaa juu ya Bamba la Uhindi ambalo ni bamba la gandunia lililokuwa kama kisiwa kikubwa ndani ya Bahari Hindi hadi kujisukuma dhidi ya Bamba la Asia takriban miaka milioni 10 iliyopita. Mshtuko wa mgongano huu ulisababisha kukunja kwa ganda la dunia na kutokea kwa nyororo za milima ya Himalaya ambayo inazidi kurefuka kidogokidogo kila mwaka.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bara Hindi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.