Bhutan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bhutan
Bendera
Nembo
Mji mkuu (na mkubwa zaidi){{{mji_mkuu}}}
27°28′ N 89°38′ E
Lugha rasmi{{{lugha_rasmi}}}
Serikali{{{serikali}}}
{{{vyeo_viongozi}}}{{{majina_viongozi}}}
{{{muundo_uhuru}}}{{{tarehe_uhuru}}}
Eneo
 • Eneo la jumla{{{eneo_jumla}}}
 • Maji (%){{{maji}}}
Idadi ya watu
 • Kadirio la 2023{{{watu_kadirio}}}
Pato la TaifaKadirio la 2023
 • Jumla{{{pato}}}
 • Kwa kila mtu{{{pato_kwa_mtu}}}
Pato Halisi la TaifaKadirio la 2023
 • Jumla{{{pato_halisi}}}
 • Kwa kila mtu{{{pato_halisi_kwa_mtu}}}
Maendeleo ({{{mwaka_maendeleo}}}){{{maendeleo}}}
Fedha{{{fedha}}}
Majira ya saa{{{majira_saa}}}
Muundo wa tareheDD/MM/YYYY
Ramani ya Bhutan

Bhutan ni nchi ndogo ya Bara Hindi katika milima ya Himalaya.

Nchi imepakana na Uhindi na jimbo la Tibet la China.

Imetawaliwa na mfalme Jigme Singye Wanchuck tangu 1972.

Kuna wakazi takriban lakhi saba unusu.

Mji mkuu unaitwa Thimphu.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Bhutan ni nchi ya milima, na zaidi ya 80% za eneo la Bhutan ziko juu ya kimo cha mita 2,000. Kusini tu kuna kanda nyembamba ya tambarare ya Duar.

Watu walio wengi hukalia eneo la milimani kati ya mita 2,000 hadi 3,000 juu ya UB.

Mpakani kwa China kuna milima ya juu ya Lunana. Kula Kangri ni mlima mkubwa wenye kimo cha mita 7,553.

Zaidi ya theluthi mbili za nchi zimefunikwa na misitu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Bhutan ilianzishwa mwaka 1644 na mmonaki Mbuddha Shabdrung Ngawang Namgyel.

Nchi iliweza kutunza uhuru wake hadi leo, lakini ililazimishwa kukubali maeneo ya kusini yatwaliwe na Waingereza na kuunganishwa na Uhindi wa Kiingereza. Uingereza ilishughulika pia mawasiliano ya nje ya Bhutan.

Uhusiano huu umeendelea na India kulingana na mkataba wa urafiki wa tarehe 8 Agosti 1949.

Tarehe 12 Februari 1971 Bhutan ikapokelewa kama nchi mwanachama wa UM.

Wakazi na Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Mbhutan
Ngoma ya kinyago ya Bhutan

Wabhutan walio wengi huishio mlimani wako karibu kiutamaduni na kilugha na watu wa Tibet na Burma. Hao hufuata dini ya Ubuddha (74.8%) ambayo ndiyo dini rasmi. Lugha za jamii hiyo zinazotumika nchini humo ni 23. Mojawapo, Kidzongkha, ndiyo lugha rasmi.

Watu wa kusini wanafanana zaidi na watu wa Nepal na hutumia Kinepali, mojawapo ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Wanafuata dini ya Uhindu (22.6%).

Bhutan inajitahidi kutunza utamaduni wake. Hadi mwaka 1974 watalii hawakuruhusiwa kutembelea nchi. Baadaye imewezekana lakini si rahisi kupata kibali.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Bhutan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.