Nairobi
| Nairobi | |||
| Kitovu cha mji wa Nairobi | |||
|
|||
| Mahali pa mji wa Nairobi katika Kenya | |||
| Anwani ya kijiografia: 1°17′S 36°49′E / 1.283°S 36.817°E | |||
| Nchi | Kenya | ||
|---|---|---|---|
| Mkoa | Nairobi | ||
| Wilaya | Nairobi | ||
| Idadi ya wakazi (2009) | |||
| - Mji | 3,138,295 | ||
| Tovuti: www.citycouncilofnairobi.go.ke | |||
Nairobi ni mji mkuu wa Kenya na vilevile mojawapo ya mikoa ya Kenya. Ni kati ya miji mikubwa ya Africa ukiwa na wakazi wapatao milioni 3. Kulingana na sensa ya 2009, Nairobi ina wakaaji 3,138,295 katika eneo la 696 km2 (269 sq mi). Pamoja na votongoji vyake, Nairobi ni mji wa 12 kwa ukubwa barani Africa Jina Nairobi limetokana na neno la Kimaasai, Enkarenairobi, linalomaanisha "mahali penye maji baridi."
Lugha zote za Kenya huzungumzwa Nairobi lakini hasa ni Kiingereza na Kiswahili, pamoja na Sheng.
Yaliyomo |
Eneo lake, hali ya hewa [hariri]
Nairobi imeanzishwa mahali ambako nchi tambarare ya Athi inakutana na mtelemko wa nyanda za juu zinazoongozana na Bonde la Ufa. Kitovu cha Nairobi iko zipatao 1624 m juu ya UB. Mahali pake ni kama 150 km kusini mwa ekweta. Hali ya hewa haina joto kali. Halijoto ya wastani ni 20,5° mwezi wa Machi, na 16,8° mwezi wa Julai. Mvua nyingi hunyesha mwezi wa Machi (199 mm), kiangazi ina 14mm tu wakati wa Julai.
Mitaa ya Nairobi [hariri]
Ndani ya jiji la Nairobi kuna mitaa mbalimbali kama vile Dandora, Eastleigh, Embakasi, Highridge, Huruma, Jericho, Karen, Kariobangi, Kiambiu, Kibera, Langata, Lavington, Mathare, Parklands, South C, Westlands, Kawangware Karen
Historia ya Nairobi [hariri]
Nairobi imeanzishwa mw. 1899 na Waingereza kama kambi ya kujenga Reli ya Uganda. Mahali ilikuwa karibu katikati ya Mombasa na Kampala, palikuwa na maji ikaonekana ilifaa kwa kituo njiani. Mwanzo wa Nairobi ilikuwa kambi kubwa ya hema na ghala za vifaa vya kujenga reli. Mwanzoni viongozi wengine walitaka kuacha eneo hili kwa sababu ya matope mengi. Lakini makao iliendelea kukua nyumba za mawe zikajengwa. Mw. 1905 Waingereza walihamisha ofisi kuu ya serikali yao ya kikoloni kutoka Mombasa kwenda Nairobi ikawa makao makuu ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (British East Africa war, baadaye Kenya Colony).
1963 ikawa mji mkuu wa nchi huru ya Kenya.
Ikaendelea kukua haraka.
Nairobi ya leo [hariri]
Nairobi imeibuka kuwa mojawapo ya miji mikubwa katika bara la Africa. Mashirika mengi makubwa duniani yamefungua ofisi zao zinazoshuhudia eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika ya Kati. Mojawapo ya mashirika haya ni ofisi za ya tawi la Umoja wa Mataifa (United Nations), UNEP. Kunazo pia ofisi za mabalozi wa nchi mbali mbali duniani. Nairobi, kama miji mingi mikubwa, ina matatizo mengi yanayotokea kwa sababu ya ukubwa wake. Watamaduni walioupanga mji wa nairobi hawakutegemea kuwa ungenenepa hivyo. Wataalamu wengi wametoa maoonyo mengi kuhusu ukubwa wa mji huu na uwezo wake wa kuwahudumia waakaazi wote ambao wanazidi kuongezeka kila mwaka. Nairobi imewavutia waakaazi wengi wote wakiwa na hamu ya kujitafutia riziki yao. Ijapokuwa kunao wanaofanikiwa, wengi wao hujipata wameangulia patupu wakawachwa bila pesa au hali ya kujikimu. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa wakaazi wa maeneo yasiyotengwa wananchi, maarufu kama 'slums' kwa kimombo. Eneo kubwa zaidi jijini Nairobi ni Kibera. Eneo hili lina ukubwa wa kilomita 2 kwa 2 na wakaazi takribani milioni moja. Eneo hili halina mipango yeyote ya kuruhusu binadamu kuishi lakini umaskini umewavutia wengi kuishi kule.
Kunayo pia matatizo ya ujambazi wa kibinafsi, ujambazi wa nyumba na utekaji nyara wa magari. Matatizo haya yamesababisha watu wengi kutoupendelea mji wa Nairobi.
|
|