Kifaru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Faru
Rhino-216.jpg
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Perissodactyla
Familia: Rhinocerotidae
Gray, 1820
Jenasi: Ceratotherium Gray, 1868

Dicerorhinus Gloger, 1841
Diceros Gray, 1821
Rhinoceros Linnaeus, 1758

Vifaru au faru ni wanyamapori wakubwa wa familia Rhinocerotidae. Spishi wawili kati ya hawa wanapatikana Afrika na wengine watatu huko Asia. Huko India wamebaki faru 2700 tu na hata faru weupe nao wameadimika sana duniani.

Faru hufahamika sana kwa umbo lake kubwa (ni miongoni mwa wanyama wala nyasi waliobakia); huku kila spishi ya faru ikikaribia kuwa na uzito wa tani moja na ngozi ngumu ya kujilinda, yenye unene was m 1-5-5; ubongo mdogo wa mamalia (gramu 400-600) na pembe kubwa. Wao hula sana majani. Faru wa Afrika hukosa meno ya mbele na na kutegemea zaidi magego katika kusaga chakula.

Faru huthaminiwa sana kutokana na pembe zao. Pembe hizo zimetengenezwa kwa keratini, protini, sawa na ile inayopatikana iliyotengeneza kwenye nywele na kucha. [1] Faru wa Afrika na Sumatra wana pembe mbili huku wale wa India na Java wakiwa na pembe moja tu. Faru wana uwezo mkubwa wa kusikia na kunusa,lakini uoni wao si mzuri sana. Weusi huishi kwa miaka 60 na zaidi.

Yaliyomo

Uanishaji na utoaji wa majina.[hariri | hariri chanzo]

Neno ‘rhinoceros’ ambalo ni la kimombo lenye maana ya faru/ kifaru limetokana na lugha ya Kigiriki, ‘rhino-, rhis’ maana yake pua na ‘keras’ maana yake pembe.

Kuna spishi tano zinazoweza kuwekwa kwenye makundi matatu. Spishi mbili za Afrika, faru mweupe, "White Rhinoceros" na 'faru mweusi", "Black Rhinoceros", walitokea kama miaka milioni 5 hivi iliyopita. Tofauti kubwa kati ya faru mwepe na faru mweusi ni muundo wa midomo yao. Faru weupe wana midomo mipana kwa akili ya kula nyasi huku midomo ya faru weusi ikiwa iliyo iliyochongoka kiasi.

Faru mweupe[hariri | hariri chanzo]

Faru mweupe huyu, White Rhinoceros, kimsingini wa kijivu

Faru weupe kwa muonekano wa ni wa kijivu. Maana ya neno weupe ilikosewa tu kutokana na neno la kiholanzi ‘wijd’ lenye maana ya upana ‘wide’ ambalo lilizoeleka kama ‘white’ ambalo sasa laeleweka hivyo kama mweupe. Aliitwa hivyo kwa maana ya upana, sababu wa mdomo wake mpana wenye umbo la mraba.

Faru mweupe ndiyo mnyama mkubwa wa ardhini baada ya tembo. Anakaribiana kidogo na na Faru wa India na Boko. Faru weupe wana mwili uliojaa, na kichwa kikubwa, shingo fupi na kifua kipana. Faru anaweza kuzidi uzito wa kiligramu 3,500 na urefu wa mita 3.5 – 4.6 kuanzia kichwani na mabega ya urefu wa sentimeta 180 – 200. Uzito wa faru mweupe ukovunja rekodi ni ule wa kilogramu 4,600. [2]Ana pembe mbili huku ile ya mbele ikiwa kubwa zaidi hata kufikia urefu wa sentimeta 90 -150. Faru weupe pia wana nundu kubwa inayoshikilia vichwa vyao vizuri. Huwa na nywele kadhaa hasa kwenye masikio yao na mkiani, sehemu nyingine za mwili zikiwa zimesambaa kidogo tu.

Faru mweusi[hariri | hariri chanzo]

Faru mweusi ana mdomo uliochongoka.

Faru weusi wana mdomo uliochongoka. Wanafanana kwa rangi na faru weupe. Hii inachanganya sana, sababu majina yao ni tofauti lakini rangi zao ni sawa kabisa. Spishi hii ina spishi nyingine nne ndani yake. Faru mkubwa mweusi huwa na urefu wa sentimeta 150 – 175 [3] mabegani mwake na urefu wa meta 3.5 – 3.9 mabegani mwake. Huwa na uzito wa kiligramu 850 mpaka 1600, na wachache mpaka kg 1800, huku faru jike wakiwa na umbo dogo kiasi kuliko wanaume. Pembe kubwa mbili zimetengenezwa kwa keratini huku ile kubwa ya mbele likiwa lina urefu wa mpaka sentimeta 50, na mmoja aliwahi hata kufikia sentimeta 140. Wakati fulani hata pembe la tatu hujitokeza. Faru weusi ni wadogo kiasi kuliko faru weupe, na wana mdomo uliochongoka kwa ajili ya kukusanya majani kabla ya kula.

Faru wa India[hariri | hariri chanzo]

Faru wa India na mwanae.
Sanamu ya Faru wa shaba, wa Western Han (202 K.K – 9 BK) nyakati za China

Faru hawa wa India hasa wanapatikana sana huko Nepall na hasa kaskazini – Masharikimwa India. Sasa wanapatikana Pakistan mpaka Bama na wamefika hadi China. Lakini kutokana na mwingiliano wa binadamu, uwepo wao umeathirika na wameanza kupungua. Ngozi yao pana ya kahawia karibu na kijivu yenye mikunjo. Juu ya miguu yao na mabega yao kuna vijinundu, na wananywele kidogo kwenye miili yao. Faru dume huwa wakubwa kiasi kuliko faru jike kufikia uzito wa kilogramu 2500 – 3200. Faru jike wa india hufikia mpaka uzito kilogramu 1900. Faru hawa hufikia mpaka urefu wa mita tatu mpaka nne. Faru hawa wana urefu wa sentimeta 20 mpaka 101, karibu theruthi mbili ya faru wote waliobaki duniani, wanapatikana katika mbuga ya Taifa Kaziranga huko India.

Faru wa Java[hariri | hariri chanzo]

Hawa ndio mamalia wakubwa waliohatarini kutoweka. Mpaka mwaka 2002, walikuwa wamebaki faru 60, huko Java Indonesia na Vietnam. Hii ndio spishi ndogo kuliko wote. Wanyama hawa wanapenda kukaa kwenye misitu ya mvua, nyasi ndefu na maeneo yenye mafuriko ya hapa na pale na matope.

Faru wa Java pia wana pembe moja. Pia ngozi yao ya kijivu ina mikunjo na wana nundu kama faru wa India, na hawana nywele. Urefu wa mwili wake ni mita 3.1 – 3.2, pamoja na kichwa na urefu wa mita 1.5 – 1.7. faru wakubwa hufikia uzito wa kilogramu 900 – 1400 [15] au 1360 – 2000. Pembe za faru dumenhufikia mpaka sentimeta 26 huku faru jike huwa na nundu tu, na wakati mwingine hawana kabisa.

Faru wa Sumatra[hariri | hariri chanzo]

Faru wa Sumatra huko Bronx Zoo

Hawa ndio faru wadogo kabisa katika sishi zote za faru na ndiye huyu pekee mwenye manyoya mengi na nayeweza kuishi katika sehemu za juu hasa za Borneo na Sumatra. Kutokana na kuharibika kwa makazi yao na ujangili, wameadimika sana na miongoni mwa mamalia walioadimika sana. Mpaka sasa inaaminika sana kwamba wamebaki faru 275 wa spishi hii.

Faru wa Sumatra wana kimo cha urefu wa sentimeta 130 mpaka mabegani, na mwili wake wa urefu sentimeta 240 – 315, na wana uzito wa kilogramu 700, japo baadhi yao wana uzito hata kufikia kilogramu 1000. Kama faru wa Afrika, hao wana pembe mbili zenye urefu mpaka sentimeta 25 – 27 na ile pembe ya pili ni ndogo na huwa ndogo kufikia sentimeta 10. Pembe za faru dume wana pembe kubwa kuliko faru jike. Nywele / manyoya ya miili yao hupungua kadri wanavyoongezeka umri. Rangi ya Faru hawa ni kahawia – nyekundu. Mwili wao ni mfupi na miguu yao pia na midomo yao ina nguvu sana.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]