Chakula
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Aina za nyama.
Chakula ni kile kinacholiwa na watu kwa kudumisha maisha yao. Mwili unahitaji lishe, nishati na maji. Haya yote hupatikana katika chakula.
Mahitaji ya mwili ni hasa yafuatayo:
- protini
- mafuta
- wanga (kabohidrati)
- vitamini na madini.
Protini, mafuta na wanga huleta nishati kwa mwili. Vilevile hukuza mwili yaani tumboni zinapasuliwa katika sehemu asilia zao na kuingizwa katika muundo wa seli za mwili.
Chakula kinatoka kwenye mimea na pia kwenye wanayama. Sehemu ya mahitaji yanatoka pia moja kwa moja kwenye mazingira bila kupita mimea au wanyama hasa madini kwa mfano chumvi.
Lakini chakula si pekee kazi ya kibiolojia na kifiziolojia kina upande wa kiutamaduni na kijamii vilevile.
Kila nchi ina chakula chake na watu wamezoea vyakula pamoja na namna ya kutayarisha vyakula vyao.
| Vyakula vya kibinadamu | ||
| Asili ya mimea' | Asili ya wanyama | |