Meru, Kenya
| Meru | |
| Mahali pa mji wa Meru katika Kenya | |
| Anwani ya kijiografia: 0°3′0″N 37°39′0″E / 0.05°N 37.65°E | |
| Nchi | Kenya |
|---|---|
| Mkoa | Mashariki |
| Wilaya | Meru Kati |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 140,900 |
| Tovuti: www.merutown.com | |
Meru ni mji wa Kenya katika Mkoa wa Mashariki. Mji wa Meru ni makao makuu ya Wilaya ya Meru Kati katika Jimbo la Mashariki na mji wa nane kwa ukubwa nchini Kenya. Meru imeunda baraza ya minispaa na wakazi 140,900 [1]
Meru iko pande za Mto kathitaṃ, katika mteremko wa kaskazini mashariki wa Mlima Kenya. Mji huuuko umbali wa maili tano kaskazini mwa ikweta, urefu wa futi 5000, katika eneo la mchanganyiko wa misitu mahali wazi, miji midogo, vijiji, mashamba vijijini na wengi wa wakazi niwa Ameru.
Unaweza kufika mji huu ukitumia barabara ya lami ,kwa vyovyote vile kama kutoka kusini kuzunguka upande wa mashariki wa Mlima Kenya, kupitiaEmbu, au kutoka katika eneo la kaskazini magharibi kuzunguka magharibi na kaskazini wa Mlima Kenya, kupitia Nanyuki na Timau (Tangu Februari As of 2004[update] barabara ya Meru kupitia Nanyuki haikuwa sawa). Wilaya ya Meru ni mahali pa kuzuru li kutembelea eneo za kuhifahia wanyama ambazo ni Samburu na Buffalo Springs Lewa Downs, ambazo ziko mbali kiasi kaskazini mwa Meru, pamoja na Samburu na Buffalo Springs kupitia Isiolo, na mbuga wa waanyama Meru, katika kaskazini ya Meru, kupitiaMaua katika vilima vya Nyambeni.
Meru ni mji wa biashara, kilimo na elimu kaskazini ya Kenya. Mji huu uko na mabenki na hoteli , masoko na vituo vya usafirishaji. Kahawa, chai, mbao, ng'ombe, maziwa, maharagweya"Kifaransa" na bidhaa nyingine nyingi hutoka katika Wilaya ya Meru. Pia kuna shule za msingi na sekondari, zikiwa pamoja na Shule kuu ya sekondari ya Meru na shule ya wasichana ya kaaga, ambazo ni baadhi ya chuo zinazoongoza katika taasisi za elimu ya sekondari Kenya. Chuo kikuu cha Emory ina ubia na Shule kuu ya sekondari ya Meru katika kusidiana na kompyuta, vitabu, na vifaa vya sayansi katika kumbukumbu ya George Brumley. Pia kuna shule za Ufundi. Taasisi ya ufundi Meru na Chuo cha Teknolojia ya Meru ambazo ndizo kuu. Pia, kuna vyuo vya ualimu na chuo kikuu cha Kenya Methodist University kinachojulikana kama KEMU.
Ni eneo muhimu la uzalizaji wa kahawa. inakuzwa na wengi wa wakulima wadogo, nakukuzwa chini ya kivuli. Mazao ya kahawa katika eneo la Meru huja mara mbili kwa mwaka, sawa n misimu miwili ya mvua, lakini mazao kuu katika Meru inakuja katika wakati tofauti kwa kiasi fulani kuliko mahali pengine nchini Kenya, kutokana na tofauti ya hali ya hewa kwenye kaskazini wa miteremko ya mlima Kenya na vilima vya Nyambenene . pia hukuzwa katika miinuko iliyo juu katika mchanga wa volkeno katika wilaya hii. Kahawa hii inatayarishwa na vyama vya ushirika vya wakulima wa kahawa ambavyo ni wenyewe viwanda vilivyo karibu na wakulima.
Meru ndio eneo kuu la ukuzaji wa Miraa (Khat) nchini Kenya. Wakulima wengi wanapendelea kuzalisha miraa kwa kuwa ina faida kubwa kifedha.
Makumbusho ya Taifa ya Meru liko katika mji.
Orodha ya hoteli katika Meru [hariri]
- Hotel Incredible
- Blue towers Hotel
- White Star Hotel
- Three steers hotel
- Meru County Hotel
- Meru Safari Hotel
- Hotel ya Royal Prince
- Simba Wells
- Timau River Lodge
Orodha ya Wameru maarufu [hariri]
- Field Antioch Musa Mwariama, Mau Mau Kiongozi
- Mhe. Justice (RTD) Aaron Ringera, sasa Mkurugenzi Kenya Anti-Corruption Commission (KACC), Kenya [1]
- Francis Muthaura, sasa Katibu Mkuu wa hudumawa za umma na Baraza la Mawaziri, Kenya.
- Edward H Ntalami, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa haraka, Capital Markets Authority, Kenya.
- David Mwiraria, aliyekuwa Mbunge wa Imenti ya Kaskazini aliyekuwa Waziri wa Mazingira na Mali asili, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Kenya.
- Kiraitu Murungi,mbunge na sasa wa imenti kusini naWaziri wa Nishati, Kenya.
- Samuel Kobia, Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa (WCC). [2]
- Sila Muriuki,Mbunge wa sasa (tangu Desemba 2007 uchaguzi) wakwa Imenti kaskazini,(Chama cha mazingira ch Kenya).
- Mbiuki Japhet Kareke, sasa mbunge waNithi, na mfanyabiashara maarufu. wa mabasi na malori.
- Gitobu Imanyara, sasa Mbunge wa Imenti ya Kati, aliyekuwa mwanaharakati wa kisiasa, aliyekuwa Katibu Mkuu wa FORD-Kenya
- Kilemi Mwiria], sasa mbunge wa Tigani-Magharibi na Naibu Waziri wa Elimu ya juu, kwa chuo kikuu cha KKU na mhadhili wa shughuli za UNCEF za elimu ya watoto katika Afrika.
- Peter Munya mbunge wa Tiagnia-Mashariki
- Abdul Aziz Dawood, wenye kiti wa baraza ya mji wa Meru. Mwanabiashara ambaye ana vituo vya mafuta na hoteli.
- Isaka Kaimenyi Ndiira, OCPD Mstaafu na mkuu wa zamani wa afisa wa usalama katika kampuni ya Mabati Rolling Mills, ambayo ndiyo kampuni inayoongoza katika utengenezaji wa mabati Afrika Mashariki na Kati.
- Jackson Harvester Angaine -1900-1999 Aliyekuwa Waziri wakati wa Kenyatta na Moi
- Nteere Mbogori -1934-2008 mbunge wa zamani wa Imenti Kaskazini , Naibu Waziri wakati wa utawala wa Moi , na mmoja wa mwanzilishi wa GEMA
- Askofu lawi Imathiu - Askofu wa zamani wa Methodist
- Maore Maoka - mbunge wa zamania wa Ntonyiri
- Mheshimiwa Justus Tom Ndege Sabari 1946-2008. Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Wizara ya Mambo ya ndani, Wizara ya Mazingira na mali asili. Mwanachama mwanzilishi wa chuo kikuu cha Methodist - Meru.
Marejeo [hariri]
- ↑ Kenya National Bureau of Statistics: Wakazi wa serikali za mitaa
| Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Meru, Kenya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |