Garissa
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Garissa | |
| Mahali pa mji wa Garissa katika Kenya | |
| Anwani ya kijiografia: 0°27′25″S 39°39′30″E / 0.45694°S 39.65833°E | |
| Nchi | Kenya |
|---|---|
| Mkoa | Kaskazini-Mashariki |
| Wilaya | Garissa |
| Idadi ya wakazi | |
| - Mji | 65,881 |
Garissa iko upande wa mashariki ya Nairobi
Garissa ni mji nchini Kenya mwenye wakazi 65,000 na makao makuu ya Mkoa wa Kaskazini-Mashariki. Mto Tana hupita eneo la manisipaa.
Wakazi walio wengi ni Wasomalia kiutamaduni pamoja na raia wa Somalia waliohamia hapa kutokana na hali ya vita nchini humo. Kundi kubwa la wenyeji ni ukoo wa Waogaden.