Kahawa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa maana nyingine ya jina hili angalia Kahawa (maana)

Kikombe cha kahawa.

Kahawa ni kinywaji kinachotengezwa kutokana na buni ambazo ni mbegu za mbuni.

Kahawa ni kinywaji kinachozidi kuenea duniani. Inapendwa kwa sababu ya ladha yake pamoja na dawa ya kafeini iliyomo ndani yake. Kafeini ina taathira ya kuchechemua na kuondoa uchovu.

Matumizi ya kahawa[hariri | hariri chanzo]

Kuchemsha unga wa kahawa pamoja na maji ni njia asilia ya kutengeneza kinywaji hicho.

Wanywaji wakuu wa kahawa duniani ni watu wa Ufini wanaotumia kilogramu 11.3 kwa mwaka kila mkazi, ambayo ni sawa na vikombe 1,737 kwa mwaka au vikombe 5 kwa siku kwa kila mkazi. Lakini watoto hawanywi kahawa, hivyo watu wazima hunywa zaidi kuliko wastani huu.

Wakazi wa Marekani katika mwaka 1998 walitumia kahawa tani 1.148.000 inayolingana na wastani wa matumizi ya vikombe 1.8 kwa siku kila mkazi.

Wajerumani huwa na wastani wa vikombe 4 kwa siku; hii ni zaidi kuliko matumizi yao ya bia.

Kahawa kwa kupunguza uzani mwilini[hariri | hariri chanzo]

Wanaouza dawa za kupunguza uzani husema kwamba kafeini iliyomo katika kahawa huchangia katika kuyeyusha mafuta. Hili hufanyika wakati mwili unapotoa joto. Katika ile hali ya kutoa joto (thermogenesis) mafuta huyeyushwa na kufanywa kawi. [1] Hata hivyo, hili laweza kuchangia upotevu wa usingizi wakati wa usiku pamoja na kuwa na fadhaiko (anxiety)

Njia za kutengeneza kahawa[hariri | hariri chanzo]

Buni zilizokaangwa hupondwa au kusagwa kuwa unga wa kahawa. Mara nyingi kipimo ni kijiko kidogo kimoja cha unga kwa kila kikombe cha kahawa. Watu wengi wanakoroga sukari au maziwa katika kahawa kulingana na mapenzi yao.

Kuna njia mbalimbali za kutengeneza kahawa zinazotofautiana kati ya nchi na nchi.

  • Espresso: unga huwekwa katika chujio ndani ya mashine na maji ya kuchemka hupitishwa kwa shindikizo katika unga. Asili ya mashine hizi ni Italia lakini zimeenea duniani. Kahawa yake ni nzito lakini inakorogwa mara nyingi pamoja na maziwa au povu la maziwa. Utamu wa kahawa ya espresso hulingana si tu na ubora wa buni, bali pia na ubora wa mashine ya kutengenezea espresso.
  • Kahawa ya filta: unga huwekwa katika mfuko wa karatasi ya filta juu ya birika na maji ya kuchemka humwagwa juu yake yakitirikika chini polepole. Kuna pia filta za metali. Mara nyingi watu wanatumia machine wakijaza unga kwenye filta na maji kwenye chombo cha mashina na kuwasha mashine tu inayochemsha maji yanayotiririka polepole kuingia katika filta.
  • Kuna pia birika au mashine zinazoiga mwendo wa espresso lakini bila shindikizo kali hivi. Kwa mfano kuna birika ambako unga na maji ya kuchemka zinamwagiwa pamoja. Mchanganyiko unakaa kwa dakika moja au mbili, halafu kuna chujio kwenye mfuniko wa birika inayosukumwa chini polepole. Unga unashikwa chini na kahawa inapita kukaa juu.
  • Kahawa mumunyifu: inatengenezwa kwa kutumia unga wa pekee ulioandaliwa kiwandani. Hapa kahawa inatengenezwa kiwandani halafu maji huondolewa kwenye kahawa na unga unabaki unaokorogwa tu katika maji ya moto na kahawa ni tayari. Watu wengi wameizoea kwa sababu inatengenezwa haraka lakini wapenzi wa kahawa mara nyingi wanalalamika ya kwamba sehemu ya ladha inapotea.
  • Kahawa latte (coffee latte): jina hutokana na neno la Kiitalia "latte" (maziwa); hutengenezwa kwa kuchukua aina ya kahawa, kuitengeneza espresso na kuweka maziwa ndani. Kwa hiyo, tofauti na espresso ni kuwa huwa na maziwa.

Picha[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Makala ya Webmd yaonyesha kwamba kafeini huinua joto mwilini kutoka asilima ishirini na nane hadi sabini na saba.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]



Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kahawa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.