Ufini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Suomen tasavalta
Republiken Finland

Jamhuri ya Ufini
Bendera ya Ufini Nembo ya Ufini
Bendera Nembo
Wito la taifa: none
Wimbo wa taifa: Maamme (Kifini)
Vårt land (Kiswidi)
("Nchi yetu" Kiswahili)
Lokeshen ya Ufini
Mji mkuu Helsinki
60°10′ N 24°56′ E
Mji mkubwa nchini Helsinki
Lugha rasmi Kifini, Kiswidi
Serikali Jamhuri2
Sauli Niinistö
Jyrki Katainen
Uhuru
imetangazwa
6 Desemba 1917
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
338,145 km² (ya 64)
9.4
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2000 sensa
 - Msongamano wa watu
 
5,265,926 (ya 112)
5,181,115
15/km² (ya 190)
Fedha Euro (€)1 (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD [.fi]
Kodi ya simu +358

-

1Prior to 1999: Finnish markka
2Semi-presidential systemUfini (pia: Finland, Finlendi; Kifini: Suomi) ni nchi ya Skandinavia au Ulaya ya Kaskazini. Pia ni nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Imepakana na Norwei upande wa Kaskazini, Urusi upande wa mashariki na Uswidi upande wa magharibi. Ng'ambo ya Baltiki iko Estonia na watu wake hutumia lugha iliyo karibu sana na Kifini.

Mji mkuu ni Helsinki. Nchi ina wakazi milioni tano tu katika eneo la 338,000 km² hivyo ni kati ya nchi za Ulaya zenye msongamano mdogo wa watu. Sehemu kubwa ya eneo lake ni misitu tu.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Kuna jumuiya tatu katika Ufini: Wafini wenyewe ambao ni 92% ya wakazi wote. Waswidi wako hasa upande wa kusini mwa nchi kwa jumla takriban 5.5% ya wakazi. Hasa visiwa vya Aland kuna Waswidi watupu walio na hali ya kujitawala ndani ya Ufini. Wakazi asilia ni Wasami wako kaskazini tu. Maisha yao yanategemea uwindaji na ufugaji. Wako wachache, jumla yao haifiki 1% ya wakazi wote.

Lugha rasmi ni Kifini na Kiswidi. Lugha ya Kifini ina asili ya Asia ya kati haina uhusiano na lugha nyingine ya Kiulaya isipokuwa lugha ya Waestonia inafanana. Inaonekana ya kwamba mababu wa Wafini na Waestonia walihama pamoja wakiwa na lugha ileile zamani lakini sasa ni lugha mbili kwa sababu hawakuwa na mawasiliano kati yao kwa muda mrefu.

Wakazi wenye lugha ya Kiswidi wako upande wa kusini mwa nchi kwa sababu Ufini ilitawaliwa na Uswidi kwa karne nyingi. Katika karne hizi walikuwepo Waswidi waliohamia Ufini lakini kuna pia Wafini walioanza kutumia Kiswidi pekee. Hasa kwenye visiwa vya Aland Kiswidi ni lugha ya pekee. Lakini Waswidi wa Ufini wanajisikia wako Wafini kisiasa. Viongozi wa kwanza baada ya uhuru wa Ufini mwaka 1917 walikuwa Waswidi Wafini.

Waja[hariri | hariri chanzo]

Links[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ufini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.