Ukraine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Україна
Ukrayina

Ukraine
Bendera ya Ukraine Nembo ya Ukraine
Bendera Nembo
Wito la taifa: --
Wimbo wa taifa: Ще не вмерла України
Shche ne vmerla Ukrajiny]]
"Ukraine's glory has not perished"
Lokeshen ya Ukraine
Mji mkuu Kiev (Kyiv)
50°27′ N 30°30′ E
Mji mkubwa nchini Kiev
Lugha rasmi Kiukraine
Serikali Demokrasia
Viktor Yanukovych
Mykola Azarov
Uhuru
ilitangazwa
Kura ya maoni ya wananchi
ilikubaliwa
24 Agosti 1991
1 Desemba 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
603,700 km² (ya 44)
7%
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
46,481,000 (ya 27)
48,457,102
77/km² (114th)
Fedha Hryvnia ya Ukraine (UAH)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD .ua
Kodi ya simu +380

-


Ramani ya Ukraine

Ukraine (Україна}}, Ukraina) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki. Imepakana na Urusi, Belarus, Poland, Slovakia, Hungaria, Romania na Moldova.

Kuna pwani ya Bahari Nyeusi na ghuba ya Azov.

Mji mkuu ni Kiev (Kyiv).

Yaliyomo

Lugha na utamaduni [hariri]

Kiukraine (українська мова "ukrajin's'ka mova") ni lugha rasmi, lakini angalau nusu ya wakazi hutumia Kirusi. Kiukraine ni lugha ya Kislavoni karibu sana na Kirusi.

Kwa muda mrefu Ukraine ilitawaliwa na Urusi na Kirusi kilikuwa lugha ya utawala hali halisi. Tangu uhuru serikali imeendesha sera ya kujenga lugha ya kitaifa.

Wakazi [hariri]

Sensa ya mwaka 2001 ilionyesha ya kwamba 77% za wakazi hujiita "Waukraine". Waliojiita Warusi walikuwa 17%. Vikundi vingi vingine kama Wabelarus, Wamoldovia, Watartari, Wabulgaria, Wapoland, Wayahudi na wengine walikuwa kila kimoja chini ya 1%.

Walio wengi ni Wakristo wa Kanisa la Kiorthodoksi la Russia, lakini Waorthodoksi wengine wamejitenga na kuanzisha Kanisa la Kiorthodoksi la Ukraina.

Pia kuwa waamini wengi wa Kanisa Katoliki, hasa wa Kanisa Katoliki la Ukraina linalofuata mapokeo ya Mashariki kama Waorthodoksi]], lakini pia wa Kanisa la Kilatini.

Historia [hariri]

1922 - 1991 Ukraine ilikuwa jamhuri mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti na kabla ya hayo sehemu ya Dola la Urusi. Miaka 1918 - 1921 baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na ya kuporomoka kwa Dola la Urusi nchi ilikuwa na kipindi kifupi cha uhuru na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Viungo vya nje [hariri]