Hungaria
|
|||||
| Wito la taifa: -- | |||||
| Wimbo wa taifa: Himnusz ("Isten, áldd meg a magyart") "Wimbo" ("Mungu wabariki Wahungaria wote") |
|||||
| Mji mkuu | Budapest |
||||
| Mji mkubwa nchini | Budapest | ||||
| Lugha rasmi | Kihungaria (Magyar) | ||||
| Serikali | Serikali ya kibunge Jamhuri Pál Schmitt Viktor Orbán |
||||
| Uhuru Principality of Hungary Ufalme wa Hungaria Kuachana kwa Milki ya Austria-Hungaria Jamhuri ya Hungaria |
896 Desemba 1000 1918 1989 |
||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
93,030 km² (ya 109) 0.74% |
||||
| Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
10,076,581 (ya 79) 10,198,315 109/km² (ya 92) |
||||
| Fedha | Forint ya Hungaria (HUF) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CET (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
| Intaneti TLD | .hu 1 | ||||
| Kodi ya simu | +36 |
||||
| 1 pia .eu kama nchi ya Umoja wa Ulaya | |||||
Hungaria (Magyarország) ni nchi ya Ulaya ya Kati. Mji mkuu ni Budapest. Nchi ina wakazi milioni 10. Imepakana na Austria, Slovakia, Ukraine, Romania, Serbia, Kroatia na Slovenia.
Miji muhimu baada ya Budapest ni Miskolc, Debrecen, Szeged, Pécs, Győr na Szolnok.
Kihungaria ni lugha rasmi.
Yaliyomo |
Historia [hariri]
Hungaria ilitokea kama nchi ya pekee wakati wa karne ya 10 BK. Tangu zamani za kuzaliwa kwake Kristo (milenia ya kwanza) sehemu kubwa ya Hungaria ilijulikana kama Panonia ikawa sehemu ya Dola la Roma. Tangu kuporomoka kwa nguvu ya Waroma ilivamiwa na makabila mbalimbali kama vile Wagermanik, Wahunni na Waslavi.
Baada ya mwaka 900 Wahungaria chini ya mtemi Arpad walivamia eneo hili. Wakati ule Wahungaria walikuwa mkusanyo wa makabila wahamiaji waliojiita "Majari" (Magyar) waliotoka katika maeneo kati ya mto Volga na milima ya Ural. Kutoka makazi yao mapya katika Panonia waliendelea kuvamia maeneo mengine ya Ulaya hadi milima ya Pirenei. Baada ya kushindwa na Wajerumani mwaka 955 walibaki katika makazi yao na mnamo mwaka 1000 mfalme Stefano (Ishtvan) alipokea ubatizo akaongoza taifa lake kuingia katika Ukristo.
Wakati wa uvamizi wa Wamongolia baada ya Chingis Khan katika karne ya 13 nchi iliangamizwa na nusu ya wakazi wakauawa. Baadaye wafalme Wahungaria waliwakaribisha walowezi kutoka Ujerumani walioanzisha vijiji vingi na pia miji.
Wakati wa karne ya 15 Waosmani walianza kuenea kwenye Balkani wakaingia katika Hungaria kutoka upande wa mashariki. Katika mapigano ya Mohacs mwaka 1526 Hungaria ilishindwa na sehemu kubwa ikawa chini ya Waosmani. Magharibi ya nchi ikaendelea kuitwa ufalme wa Hungaria lakini ufalme uliingia mkononi mwa nyumba ya Habsburg yaani chini ya watawala wa Austria.
Katika karne zilizofuata watawala wa Habsburg walirudisha Waosmani nyuma na ufalme wa Hungaria ikawa sehemu ya milki ya Habsburg yaani Austria. Katika karne ya 19 mnamo 1848 Wahungaria waliasi dhidi ya watawala lakini walishindwa. Lakini Kaisari Franz Joseph I alibadilisha siasa akatafuta usaidizi wa Wahungaria katika utawala wa ufalme. Katiba mpya iliunda cheo cha sawa kati ya Austria na Hungaria chini ya mtawala yeye yule mwenye vyeo vya Kaisari wa Austria na Mfalme wa Hungaria na milki ikaitwa "Austria-Hungaria".
Austria-Hungaria ilikuwa milki kubwa katika Ulaya ya Kati na Mashariki kati ya 1867 hadi 1918. Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia milki ikaporomoka na Hungaria ikaendelea kama nchi ya pekee yenye katiba ya ufalme lakini bila mfalme. Katika vita kuu ya pili ya dunia Hungaria ikaingia kwa upande wa Ujerumani ukaendelea kuwatesa Wayahudi wake wa kushikamana na siasa ya Hitler na mwishowe ikashindwa pamoja na Ujerumani. Hungaria ikavamiwa na jeshi la Umoja wa Kisovyeti na mabwana hao wapya walihakikisha ya kwamba chama cha kikomunisti ilishika serikali. Hungaria ikawa sehemu ya Mapatano ya Warshawa ikasimama upande wa mashaki katika kipindi cha vita baridi. Mwaka 1956 wananchi wengi walipindua serikali ya kikomunisti na serikali mpya chini ya Imre Nagy ilianzisha demokrasia ya vyama vingi. Lakini wanajeshi wa Kisovyti wakaingia kati wakarudisha utawala wa chama cha kikomunisti ulioendelea hadi kuporomoka kwa ukomunisti mnamo 1989.
Hungaria imekuwa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya tangu 2004.
Jiografia [hariri]
Tazama pia [hariri]
Viungo vya nje [hariri]
|
||||||||||||||
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hungaria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |