Liechtenstein

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Liechtenstein
Bendera
Nembo
Mji mkuu (na mkubwa zaidi){{{mji_mkuu}}}
47°08′ N 9°30′ E
Lugha rasmi{{{lugha_rasmi}}}
Serikali{{{serikali}}}
{{{vyeo_viongozi}}}{{{majina_viongozi}}}
{{{muundo_uhuru}}}{{{tarehe_uhuru}}}
Eneo
 • Eneo la jumla{{{eneo_jumla}}}
 • Maji (%){{{maji}}}
Idadi ya watu
Pato la TaifaKadirio la 2023
 • Jumla{{{pato}}}
 • Kwa kila mtu{{{pato_kwa_mtu}}}
Pato Halisi la TaifaKadirio la 2023
 • Jumla{{{pato_halisi}}}
 • Kwa kila mtu{{{pato_halisi_kwa_mtu}}}
Maendeleo ({{{mwaka_maendeleo}}}){{{maendeleo}}}
Fedha{{{fedha}}}
Majira ya saa{{{majira_saa}}}
Muundo wa tareheDD/MM/YYYY

Utemi wa Liechtenstein (kwa Kijerumani: Fürstentum Liechtenstein) ni nchi ndogo katika Ulaya ya Kati. Imepakana na Uswisi na Austria. Ni ya sita kati ya nchi huru ndogo zaidi duniani.

Mji mkuu ni Vaduz wanapoishi wakazi 5000.

Ramani ya Liechtenstein

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Nchi yote ina urefu wa km 24.56& kutoka kaskazini hadi kusini na upana wa km 12.36.

Urefu huu unafuata mwendo wa mto Rhine ambao ni mto pekee nchini, pia ni mpaka na Uswisi.

Upande wa mashariki na karibu na mpaka wa Austria milima hupanda hadi kimo cha mita 2,599.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kwa muda mrefu nchi ilikuwa sehemu ya Dola Takatifu la Kiroma ingawa chini ya utawala wa kikabaila.

Dola hilo liliposambaratishwa na Napoleon Bonaparte (1806), Liechtenstein ilijiunga na Shirikisho la Rhein hadi mwaka 1813 ambapo lilifutwa, halafu na Shirikisho la Ujerumani (1815-1866).

Ndipo ilipopata uhuru kamili ikitegemea ulinzi kutoka Uswisi.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Lichtenstein imekuwa nchi tajiri baada ya vita kuu ya pili ya dunia kwa sababu serikali ya mtemi ilidai kodi ndogo kabisa zilizohamasisha makampuni mengi ya nje kufungua ofisi zao nchini.

Kuna pia benki nyingi zinazosemekana kuficha pesa za matajiri ambao wangetakiwa kulipa kodi ya mapato nyumbani kwao.

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Mkuu wa nchi ni mtemi Hans-Adam II anayeitwa kwa jina kamili "Johannes „Hans“ Adam II Ferdinand Alois Josef Maria Marko d'Aviano Pius von und zu Liechtenstein". Tangu tarehe 15 Agosti 2004 amemkabidhi mwanawe Alois madaraka ya utawala.

Bunge la wabunge 25 huchaguliwa na wananchi wote. Sheria zote zinapaswa kukubaliwa na mtemi. Mawaziri watano wa serikali huteuliwa na bunge na kuthibitishwa na mtemi. Wananchi wote wana haki ya kupeleka mapendekezo ya sheria, au kudai kura ya wananchi wote juu ya sheria iliyopitishwa na bunge na kuthibitishwa na mtemi.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kijerumani.

Upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki (78.4%) na Wakalvini (7.9%).

Michezo[hariri | hariri chanzo]

Tangu 1984 Liechtenstein imejiunga na FIFA na UEFA na inashiriki tangu 1994 katika uteuzi wa timu za soka katika mashindano ya kombe la Ulaya na kombe la dunia.

Hata kama nchi ya wakazi 37,000 tu, na haina klabu mashuhuri, Waliechtensetin waliweza kushtusha wapinzani wao mara kadhaa.

Mwaka 1996 klabu ya Vaduz ilishinda klabu ya Latvia FC Universitate Riga 1–1 na 4–2 lakini ilishindwa baadaye na Paris St. Germain.

Timu ya taifa ya 2004 iliweza kumaliziana na Ureno 2–2 na kushinda Luxemburg 4-0.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Liechtenstein kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.