Urusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Российская Федерация
Rossiyskaya Federatsiya

Shirikisho la Urusi
Bendera ya Russia Nembo ya Russia
Bendera Nembo
Wito la taifa: none
Wimbo wa taifa: Hymn of the Russian Federation
Lokeshen ya Russia
Mji mkuu Moscow
55°45′ N 37°37′ E
Mji mkubwa nchini Moscow
Lugha rasmi Kirusi
Serikali Jamhuri, Shirikisho
serikali ya kiraisi
Dmitry Medvedev
Vladimir Putin
Uhuru
{{{established_events}}}
{{{established_dates}}}
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
17,075,400 km² (ya 1)
13
Idadi ya watu
 - 2006 kadirio
 - 2002 sensa
 - Msongamano wa watu
 
142,400,000 (ya 7)
145,164,000
8.3/km² (ya 209)
Fedha Rubl (RUB)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+2 to +12)
(UTC+3 to +13)
Intaneti TLD .ru, (.su reserved)
Kodi ya simu +7

-

1 Rank based on Aprili 2006 IMF dataUrusi (Россия Rossiya) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki na Asia. Mji mkuu ni Moscow. Ni nchi kubwa duniani kieneo. Kuna wakazi 144,000,000. Eneo lake ni 17,075,400 km².

Hadi 1991 Urusi ilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti na kiini chake. Wakati ule iliitwa Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi. Urusi ilikuwa udikteta chini ya chama cha kikomunisti. Tangu 1990 imekuwa demokrasia. Muundo wa serikali ni shirikisho la jamhuri chini ya rais mtendaji.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Urusi imepakana na Norway, Ufini, Estonia, Latvia, Lithuania, Poland, Belarus, Ukraine, Georgia, Azerbaijan, Kazakhstan, China, Mongolia na Korea ya Kaskazini. Iko karibu vilevile na maeneo ya Marekani (jimbo la Alaska iko ngambo ya mlango wa Bering na Japani (kisiwa cha Hokkaido kiko ng'ambo ya mlango wa La Pérouse.

Eneo la Shirikisho la Kirusi linajumlisha sehemu kubwa ya kaskazini ya mabara ya Ulaya na Asia. Umbali kati ya upande wa magharibi na upande mashariki kabisa ni karibu kilomita 8,000. Mkoa wa Kaliningrad haufuatani moja kwa moja na maeneo mengine ya Urusi umetengwa nayo na nchi za Kibaltiki.

Mara nyingi Urusi hutazamiwa kama sehemu mbili za Urusi wa Ulaya hadi milima ya Ural na Siberia au Urusi wa Kiasia ambayo ni nchi pana kati ya Ural na Pasifiki. Pwani ndefu la kaskazini linatazama Bahari ya Aktiki.

Sehemu kubwa ya Urusi ni tambarare penye vilima vidogo tu. Milima mirefu kuna katika kusini na mashariki ya Siberia.

Mito[hariri | hariri chanzo]

Kati ya mito mikubwa kuna

Miji mikubwa ya Urusi[hariri | hariri chanzo]

Majiji mawili makuu ni Moscow na Sankt Peterburg. Sankt Peterburg ilikuwa mji mkuu kuanzia mwaka 1703 hadi 1918 kama makao makuu ya tsar au kaisari wa Urusi. 1924-1989 ikaitwa Leningrad kwa heshima ya kiongozi wa mapinduzi. Moscow ni mji mkuu wa kale iliyorudishwa nafasi yake baada ya mapinduzi ya kikomunisti ya 1918.

Miji mingine mikubwa ni pamoja na

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Sehemu kubwa za Urusi huwa na vipindi vya majira tofauti sana; joto kubwa inafuatana na baridi kali.

Kaskazini ya Siberia ina ardhi iliyoganda milele maana yake baridi imeingia katika ardhi kabisa. Wakati wa joto sentimita za juu zinapoa na mimea kama manyasi na maua inastawi lakini hakuna miti mikubwa kwa sababu nusu mita chini ya ardhi halijoto inakaa daima chini ya =.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Urusi kama nchi ya pekee ilianza polepole pale ambako makabila ya wasemaji wa Kislavoni cha Mashariki walipoanza kujenga maeneo yao kuanzia karne ya 8 BK. Waskandinavia waliunda dola la kwanza katika eneo la Kiev wakaitawala kama dola la Kislavoni. Wenyewe waliingia haraka katika lugha na utamaduni wa wenyeji lakini waliacha jina lao kwa sababu "Rus" kiasili ilikuwa jina kwa ajili ya Waskandinavia wale kutoka Uswidi ya leo. Mwaka 988 Kiev ilipokea Ukristo wa Kiorthodoksi kutoka Bizanti. Dola la Kiev iliporomoka kutokana na mashambulio ya Wamongolia baada ya Jingis Khan na maeneo madogo zaidi yalijitokeza yaliyopaswa kukubali uwana wa Wamongolia.

Upanuzi wa utemi wa Moscow[hariri | hariri chanzo]

Kubwa kati ya maeneo yale madogo ilikuwa utemi wa Moscow. Watemi wa Moscow walichukua nafasi ya kwanza kuunganisha Wasalvoni wa Mashariki dhidi ya Wamongolia na kupanusha utawala wao. Baada ya anguko la Konstantinopoli 1453 watawala wa Moscow walipokea cheo cha Kaisari wa Roma kilichoitwa "tsar" na kuwa cheo cha watawala wa Urusi hadi 1917.

Hadi karne ya 18 eneo ya Moscow ilikuwa tayari kubwa likabadilika kuwa Milki ya Kirusi iliyoendelea kupanua katika Siberia na Asia ya Kati. Sasa ilikuwa kati ya milki kubwa kabisa za historia ikienea kutoka Poland upande wa magharibi hadi bahari ya Pasifiki upande wa mashariki.

Matengenezo ya kisiasa chini ya Peter I[hariri | hariri chanzo]

Tsar Peter I (1689 - 1725) alitambua ya kwamba nchi yake ilikuwa nyuma kiteknolojia na kielimu kulingana na mataifa ya Ulaya. Alianzisha mabadiliko mengi ya kuiga mfano wa Ulaya ya Magharibi akahamisha mji mkuu kutoka Moscow kwenda mji mpya aliyounda sehemu ya magharibi ya milki yake akaiita Sankt Peterburg.

Tangu Peter I nchi ilishiriki katika siasa ya Ulaya pamoja na vita vingi za Kiulaya. Mwanzo wa karne ya 19 milki ikashambuliwa na Napoleon aliyeteka Moscow lakini Warusi walifaulu kuwafukuza maadui.

Upanuzi katika Asia[hariri | hariri chanzo]

Matsar wa Urusi waliendelea kutawala kwa kuwa na mamlaka zote bila kushirikisha wananchi jinsi ilivyokuwa kawaida katika sehemu nyingine za Ulaya. Miji iliona maendeleo ya viwanda na jamii ya kisasa lakini sehemu kubwa ya wakulima waliendelea kukaa chini ya utawala wa makabaila. Katika sehemu ya pili ya karne ya 19 Urusi ulipanuka utawala wake juu ya maneo makubwa ya Asia ya Kati na milima Kaukasus ikashindana na Milki ya Osmani, Uajemi na athira ya Uingereza katika Asia.

Mapinduzi za 1905 na 1917[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni wa karne ya 20 Urusi ikaonekana tena kuwa nyuma ya nchi za magharibi na sababu kuu ilikuwa nafasi kubwa ya serikali luu iliyojitahii kusimamia mabadiliko yote katika jamii na kuzuia mabadiliko iliyoonekana kama magumu machoni pa Tsar, makabaila na kanisa orthodoksi.

Mwaka 1904 upanuzi wa Urusi katika Asia uligongana na upanuzi wa Japan. Katika vita dhidi ya Japani Urusi ilishindwa na tukio hili lilisabaisha mapinduzi ya Urusi ya 1905. Tsar Nikolas alipaswa kukubali uchaguzi wa bunge la duma mara ya kwanza. Hata hivyo haki za duma zilikuwa chache na mabadiliko yalitokea polepole mno.

Urusi ilijiunga 1914 na vita kuu ya kwanza ya dunia ikisimama upande wa Uingereza na Ufaransa dhidi ya Ujerumani na Austria-Hungaria. Vita haikuenda vizuri, wananchi wakaona njaa na mapinduzi ya Februari 1917 ikamfukuza Tsar aliyejiuzulu. Vita ikaendelea na Wajerumani walizidi kusogea mbele. Serikali mpya ya bunge ikapinduliwa katika mwezi wa Oktoba 1917 na mapinduzi ya Bolsheviki chini ya kiongozi wao Vladimir Ilyich Lenin.

Utawala wa kikomunisti na Umoja wa Kisovyeti[hariri | hariri chanzo]

Hii ilikuwa mwanzo wa vita ya wenyewe kwa wenyewe. Wakomunisti chini ya Lenin walishinda na kugeuza Urusi kuwa Umoja wa Kisoveti tangu 1922 wakiitawala kwa mfumo wa kiimla wa chama chao. Ili kurahisisha utawala wao Wakomunisti waliamua kutawala Urusi ya awali kwa muundo wa shirikisho wakaunda jamhuri mbalimbali kufuatana na mataifa ndani ya eneo hili kubwa. Urusi ilikuwa sasa jina la jamhuri kubwa katika umoja huu ikaitwa Shirikisho la Jamhuri ya Kisovyiet ya Kijamii ya Kirusi.

Kikatiba jamhuri hizi zote zilikuwa nchi huria lakini hali halisi zilitawaliwa zote kutoka makao makuu ya chama cha kikomunisti huko Moscow. Katiba hii ilipata umuhimu tangu 1989 wakati wa mwisho wa utawala wa Wakomunisti ambako jamhuri zote zilitafuta uhuru wao zikaachana na Umoja. Mji mku Sant Peterburg ukabadilishwa jina kuwa Leningrad na baadaye makao makuu ya nchi yakahamishwa tena kwenda Moscow.

Kiongozi aliyemfuata Lenin 1924 alikuwa Josef Stalin aliyeweza kugeuza utawala wa chama kuwa utawala wake mwenyewe akiongoza kwa jina la Katibu Mkuu wa chama cha kikomunisti.

1939 mwanzoni wa vita kuu ya pili ya dunia Stalin alipatana na Ujerumani wa Adolf Hitler kugawa maeneo ya Poland na nchi za Baltiki kati yao lakini 1941 Hitler alishambulia pia Umoja wa Kisovyeti. Warusi walipotea askari mamilioni lakini waliweza kuwazuia Wajerumani wasiteke Moscow na Leningrad. Kwa msaada wa Marekani Warusi waliweza kurudisha jeshi la Ujerumani na kusogea magharibi. Umoja wa Kisovyeti ikawa kati ya nchi washindi wa vita kuu ya pili.

Mashindano ya vita baridi dhidi ya Marekani[hariri | hariri chanzo]

Tangu 1945 jeshi la Urusi lilikaa katika nchi zote za Ulaya ya Mashariki hadi katikati ya Ulaya. Katika nchi hozi zote serikali za kikomunisti zilianzishwa na kusimamiwa na ofisi kuu ya chama cha kikomunisti huko Moscow. Urusi ulikuwa kiongozi wa nchi za kijamii ilishindana katika vita baridi dhidi ya nchi za magharibi zilizoongozwa na Marekani. Athira ya Umoja wa Kisovyeti ilipanua hadi Afrika, Asia na Amerika ya Kati ambako nchi mbalimbali zilianza kuiga mtindo wa kikomunisti.

Kuachana kwa Umoja kwa Kisovyeti[hariri | hariri chanzo]

Utawala wa kikomunisti uliendelea hadi mnamo mwaka 1990. Mwishoni matatizo ya kiuchumi yalizidi kwa sababu mfumo wa uchumi ulioongozwa moja kwa moja na serikali kuu pamoja na utaratibu wa kiimla uliozuia wananchi kupinga siasa ya viongozi na kuleta hoja tofauti ulisababisha tena nchi kubaki nyuma.

Tangu 1990 jamhuri kadhaa za Umoja wa Kisovyeti ziliondoka katika umoja na kutangaza uhuru wao ilhali serikali ilishindwa nguvu ya kuwazuia. Mwaka 1991 jamhuri wanachama za mwisho Urusi, Belarus na Ukraine ziliamua kumaliza Umoja wa Kisovyeti.

Urusi mpya[hariri | hariri chanzo]

Tangu 1991 Urusi iliyopungukiwa na maeneo mengi yaliyotwaliwa wakati wa karne ya 19 na 18 ilibaki peke yake ingawa bdao ni dola kubwa duniani. Marais wa Urusi baada ya 1991 walikuwa Boris Yeltsin na Vladimir Putin.

Dmitry Medvedev alichaguliwa kuwa rais wa Urusi mwaka 2008 na mtangulizi wake Vladimir Putin akawa waziri mkuu.

Tovuti[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Flag-map of Russia.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Urusi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.