Ucheki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jamhuri ya Kicheki
Česká republika
Bendera ya Ucheki, Czech Nembo ya Ucheki, Czech
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Pravda vítězí
(Kicheki: "Ukweli hushinda")
Wimbo wa taifa: Kde domov můj
Lokeshen ya Ucheki, Czech
Mji mkuu Praha
50°05′ N 14°28′ E
Mji mkubwa nchini Praha
Lugha rasmi Kicheki
Serikali Jamhuri
Petr Pavel
Petr Fiala
'
Kutokea kwa taifa
Uhuru
kutoka Austria-Hungaria
Mwisho wa Chekoslovakia

Karne ya 9 (Dola la Moravia)
28 Oktoba 1918

1 Januari 1993
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
78,866 km² (ya 117)
2.0
Idadi ya watu
 - 2023 kadirio
 - 2021 sensa
 - Msongamano wa watu
 
10,827,529 (ya 85)
10,524,167
133/km² (ya 91)
Fedha Koruna (CZK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .cz 3
Kodi ya simu +4201



Ramani ya Ucheki

Ucheki au Chekia au Czechia (kwa Kicheki: Česko) pia Jamhuri ya Kicheki au Jamhuri ya Czech (kwa Kicheki: Česká republika) ni nchi ya Ulaya ya Kati na mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Imepakana na Poland, Ujerumani, Austria na Slovakia.

Mji mkuu ni Praha (Kijer.: Prag; Kiing.: Prague).

Miji mingine mikubwa ni Brno, Ostrava, Zlín, Plzeň, Pardubice, Hradec Králové, České Budějovice, Liberec, Olomouc na Ústí nad Labem.

Tangu zamani nchi imekuwa na kanda za Bohemia, Moravia na Silesia.

Wakazi husema hasa Kicheki ambacho ni lugha ya Kislavoni ya Magharibi.

Ni kati ya nchi ambako dini si muhimu kimaisha. Wakati wa sensa ya mwaka 2021, 56.9% ya wakazi walisema hawana dini yoyote, 30.1% hawakujibu swali husika, 11.7% walijitambulisha kama Wakristo (Wakatoliki 9.3% na madhehebu mengine 2.4%).

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mapema zaidi nchi ilikuwa ufalme wa Moravia kuu katika karne ya 7.

Historia ya jamhuri ya Ucheki yenyewe si ndefu, tukiangalia tangu nchi hiyo kupokea uhuru kamili mwaka 1993 hadi leo.

Hapo awali Ucheki ilikuwa imeungana na Slovakia wakiwa Cheko-Slovakia (Czechoslovakia) ambayo tena ilikuwa kwanza chini ya utawala wa ufalme wa Austro-Hungaria katika karne ya 19 hadi mwanzo wa karne ya 20, yaani mpaka vita kuu ya kwanza ya dunia wakati ufalme uliposhindwa na kusambaratika.

Rais wa kwanza kuteuliwa kwa taifa hilo mpya ni Tomáš Garrigue Masaryk.

Wakati wa vita kuu ya pili ya dunia Wajerumani walichukua uongozi wa Chekoslovakia, lakini hawakudumu mno.

Kufikia mwisho wa vita hivyo USSR ilichukua unahodha na kuweka nchi hiyo katika sera ya Ukomunisti.

Wananchi walitawaliwa kwa nguvu halisi hadi mwaka 1989 wakati kulitokea mapinduzi ya amani na kupata uhuru halisi na demokrasia.

Mwaka 1993, nchi hiyo iligawanyika katika Ucheki na Slovakia kwa sababu ya kisiasa.

Mwaka 1999 nchi ya Ucheki ilijiunga na NATO.

Ucheki imekuwa mwanachama wa muungano ya Umoja wa Ulaya kuanzia mwaka 2004.

Ucheki ni maarufu katika dunia kwa usalama wake na inapendwa sana na mamilioni ya watalii ambao huizuru kila mwaka.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Eire | Estonia | Hispania | Hungaria | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituanya | Luxemburg | Malta | Polandi | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Udeni | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ucheki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.