Majadiliano:Ucheki

Yaliyomo ya ukurasa hayatumiki katika lugha nyingine.
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Prague au Praha[hariri chanzo]

Nimetumia jina la Kicheki kwa kutaja mji mkuu, hivyo "Praha" badala ya tahajia ya Kiingereza/Kifaransa "Prague". Nadhani hakuna uzoefu sana kujadilia habari za mji huu. Tahajia ya Kifaransa (kwa sababu Waingereza walipokea tahajia ya Wafaransa walioandika kwa namna yao matamshi ya Kijerumani "Prag") haisaidii kitu. Matamshi ya "Prague" ni "Prag" lakini Mswahili anaweza kusumbuliwa na tahajia: Je "pra-gu-e"? Au "prg-we"? Ama tuandike "Prag" kama Wajerumani au tutumie jina la Kicheki "Praha". Nimeona twende kieneyeji. --Kipala 12:45, 3 Desemba 2006 (UTC)[jibu]