Umoja wa Ulaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Umoja wa Ulaya
Flag of Europe.svg
EU location.png
www.europa.eu

Umoja wa Ulaya (Kifupi: EU) ni maungano ya nchi 27 za Ulaya. Ulianzishwa mwaka 1991 kwenye msingi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya. Shabaha kuu zilikuwa kujenga uchumi wa pamoja, kuboresha maisha ya watu wa Ulaya na kuzuia vita kati ya nchi za Ulaya.

Nchi 12 za Umoja hutumia pesa ileile ya Euro, kuanzia 1 Januari 2007 Slovenia imekuwa nchi ya 13. Nchi nyingi za Umoja zilipatana kufungua mipaka yao bila vizuizi kwa wakazi wote.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jumuiya ya Kiuchumi ya Ulaya ilibadilisha jina lake 1992 kufuatana na mikataba ya Maastricht kuwa Umoja wa Ulaya. Nchi wanachama zilipatana kujenga siasa ya pamoja ya kiuchumi, kifedha, kisheria na katika mambo ya nje.

Mapatano ya Schengen ilifungua mipaka ili wakazi wa nchi hizi wanasafiri bila pasipoti wala vibali.

Nchi 10 zilijiunga tena na EU mwaka 2004. Mbili zaidi imeingia 2007.

Uhuru wa kuhama[hariri | hariri chanzo]

Kila mtu mwenye uraia wa nchi ya Umoja anaruhusiwa kuhamia nchi yoyote nyingine na kufanya kazi au biashara huko bila vibali vya pekee.

Vilevile bihdaa zote zinazotengenezwa kote katika EU zinaweza kuuzwa katika kila nchi. Hii ni sababu ya kuwa na sheria za pamoja zinazotawala masharti ya bidhaa.

Vyombo vya Umoja[hariri | hariri chanzo]

Halmashauri ya Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Halmashauri hii ni mkutano wa viongozi wa serikali za nchi wanachama. Wanakutana mara mbili kwa mwaka na kutoa maazimo muhimu.

Nafasi ya uraisi hubadilika kila baada ya miezi 6. Ufini ilishika uraisi kati ya Julai 2006 hadi Desemba 2006, ikafuatiliwa na Ujerumani tangu Januari hadi Juni 2007.

Baraza za mawaziri[hariri | hariri chanzo]

Katika baraza hizi mawaziri ya Kilimo, Sheria, Mambo ya Nje hukutana na kupanga siasa ya pamoja.

Kamati ya Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Hii ni kamati ya utawala inayotekeleza maazimio ya Halmashauri na bunge. Kuna makamishna 24 na mwenyekiti. Inaelekea kuwa serikali lakini haina madaraka ya serikali bado.

Bunge la Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Bunge la Ulaya lina wabunge 732 wanaochaguliwa na wananchi kila baada ya nchi tano.

Nchi wanachama za EU[hariri | hariri chanzo]

Nchi (jina la kienyeji - kifupi)
Austria (Österreich - AT) Bulgaria (Bălgarija - BG) Cyprus (Kypros - CY) Denmark (Danmark - DK) Eire (Éire - IE) Estonia (Eesti - EE) Hispania (España - ES) Hungaria (Magyarország - HU) Italia (Italia - IT) Latvia (Latvija - LV) Lithuania (Lietuva - LT) Luxemburg (Luxembourg - LU) Malta (Malta - MT) Polonia (Polska - PL) Romania (România - RO) Slovakia (Slovensko - SK) Slovenia (Slovenija - SI) Ubelgiji (België/Belgique - BE) Ucheki (Česká republika - CZ) Ufaransa (France - FR) Ufini (Suomi - FI) Ugiriki (Ellada - GR) Uholanzi (Nederland - NL) Uingereza (United Kingdom - UK) Ujerumani (Deutschland - DE) Ureno (Portugal - PT) Uswidi (Sverige - SE)
Wanaoomba kupokelewa: Kroatia (Hrvatska - HR) Masedonia (** - **) Uturuki (Türkiye - TR)

Wanachama tangu 1958 (waanzilishaji)[hariri | hariri chanzo]

Wanachama tangu 1973[hariri | hariri chanzo]

Mwanachama tangu 1981[hariri | hariri chanzo]

Wanachama tangu 1986[hariri | hariri chanzo]

Wanachama tangu 1995[hariri | hariri chanzo]

Wanachama tangu 2004[hariri | hariri chanzo]

Wanachama tangu 2007[hariri | hariri chanzo]

Nchi zinazoomba uanachama[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: