Marekani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka United States)
Muungano wa Madola ya Amerika
United States of America
Bendera ya Marekani Nembo ya Marekani
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: E Pluribus Unum
(kiasili "Moja kutoka wengi")
In God We Trust
(rasmi tangu 1956 "Twamtegemea Mungu")
Wimbo wa taifa: "The Star-Spangled Banner"
("Bendera ya nyota")
Lokeshen ya Marekani
Mji mkuu Washington DC
38°53′ N 77°02′ W
Mji mkubwa nchini New York
Lugha rasmi Kiingereza
hali halisi, si kisheria
Serikali Shirikisho la Jamhuri
Joe Biden
Uhuru
- Matangazo ya uhuru
- Mkataba wa Paris (1783)
Kutoka Uingereza
4 Julai 1776
3 Septemba 1783
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
9,833,517 km² (ya 31)
6.97
Idadi ya watu
 - 2016 kadirio
 - 2010 sensa
 - Msongamano wa watu
 
324,720,797 (ya 3)
309,349,689
35/km² (ya 180)
Fedha Dolar ya Marekani ($) (USD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-5 to -10)
(UTC-4 to -10)
Intaneti TLD .us .gov .edu .mil .um
Kodi ya simu +1



Muungano wa Madola ya Amerika (kwa Kiingereza: United States of America), inajulikana pia kama Marekani (kwa Kiingereza: United States, US, USA au America), ni nchi inayopakana na Kanada na Meksiko katika Amerika ya Kaskazini, mbali ya kuundwa pia na visiwa vya Hawaii.

Mji mkuu wa Marekani ni Washington DC.

Eneo

Marekani bara

Picha kutoka angani ikionyesha majimbo 48 ya Marekani yanayopakana

Eneo la Marekani lina ukubwa wa kilometa mraba 9,826,675 na liko hasa katika bara la Amerika Kaskazini kati ya Kanada upande wa kaskazini na Meksiko upande wa kusini.

Marekani imeunganisha upana wote wa bara kutoka Bahari ya Atlantiki hadi Pasifiki, ikigawanywa kwa majimbo 48 yanayojitawala.

Eneo hilo lagawiwa katikati na mto mkubwa Mississippi unaoanza mpakani kwa Kanada na kuishia katika Ghuba ya Meksiko.

Alaska

Jimbo la Alaska liko pia kwenye bara la Amerika Kaskazini upande wa kaskazini kutoka Kanada kuelekea Urusi, lakini halipakani na jimbo lolote la Marekani.

Hawaii

Funguvisiwa ya Hawaii ni jimbo la visiwani katika bahari ya Pasifiki. Ni jimbo la 50 na la mwisho mpaka sasa.

Visiwa vya ng'ambo vya Marekani

Maeneo ya ng'ambo ya Marekani ni visiwa kadhaa ambavyo ni maeneo ya Kimarekani ingawa si sehemu ya jimbo lolote. Zamani yalikuwa kama makoloni hata kama Marekani ilidai kutokuwa na ukoloni. Siku hizi maeneo haya yamepata viwango mbalimbali vya kujitawala. Kwa kawaida maeneo haya huchagua pia wawakilishi kwa ajili ya bunge la Marekani lakini wawakilishi hao si wabunge wa kawaida, bali wana haki ya kusema na kushauri tu bila haki ya kupiga kura.

Visiwa muhimu kati ya hivyo ni kama ifuatavyo:

Milima

angalia: Orodha ya milima ya Marekani

Safu ya milima ya Rocky Mountains inavuka Marekani yote kutoka kaskazini hadi kusini upande wa magharibi.

Mito

angalia: Orodha ya mito ya Marekani

Mto mkubwa wa Marekani ni Mto Mississippi.

Historia

Uenezi wa nchi hatua kwa hatua.

Nchi ilianza kama mkusanyiko wa makoloni ya Uingereza kwenye pwani ya mashariki ya Amerika ya Kaskazini tangu karne ya 17. Walowezi kutoka Uingereza walijipatia ardhi wakipigana na wenyeji Waindio.

Katika vita ya uhuru wa Marekani makoloni yalipata uhuru wao uliotangazwa mwaka 1776 na kukubaliwa na Uingereza baada ya vita mwaka 1783.

Baadaye Marekani ilipanua eneo lake hadi bahari ya Pasifiki ikatwaa ardhi ya Maindio wazalendo, ikapokea wahamiaji wengi kutoka nchi zote za Ulaya pamoja na watumwa walioletwa kutoka Afrika.

Tangu karne ya 19 wahamiaji walifika pia kutoka Asia, hasa China na Japani.

Katika vita dhidi Hispania na Meksiko, Marekani ilipanua eneo lake kwenda kusini.

Vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Marekani ilipigwa kuanzia 1861 hadi 1865 kati ya majimbo ya kusini na majimbo ya kaskazini nchini Marekani. Sababu mojawapo muhimu ya vita ilikuwa suala la utumwa. Majimbo ya kaskazini yaliwahi kupiga utumwa marufuku lakini majimbo ya kusini yaliendelea na sheria zilizoruhusu utumwa na matajiri wengi wa kusini walitegemea kazi ya watumwa. Mafarakano yalianza kuhusu swali kama madola mapya yaliyoanzishwa katika Amerika Kaskazini na kujiunga Muungano yangeruhusiwa kukubali utumwa au la. Mwaka 1861 madola ya kusini-mashariki yalitangaza kujiondoa katika Muungano na kuanzisha "Shirikisho la Madola ya Amerika". Vita ilianza na kudumu miaka minne na watu 650.000 walikufa, lakini mwishoni kaskazini ilishinda. Utumwa ulipigwa marufuku na watumwa walipewa haki za kiraia. Lakini watumwa wengi wa awali waliendelea kuwa maskini na baada ya muda, sheria mpya katika majimbo ya kusini zilinyima haki nyingi za kiraia za watu weusi waliopaswa kuishi chini mfumo wa ubaguzi wa rangi.

100 Dollars

Katika miongo iliyofuata, Marekani ilitwaa maeneo yaliyowahi kubaki chini ya mamlaka ya Waindio wazalendo na kuyafanya maeneo yake. Katika Vita ya Marekani dhidi Hispania kwenye mwaka 1898 ilijipatia utawala juu ya Ufilipino na Puerto Rico, makoloni ya awali ya Hispania, na kuwa yenyewe nchi iliyotawala makaloni.

Wahamiaji mamilioni waliendelea kufika hasa kutoka Ulaya. Kabla ya mwaka 1880 idadi kubwa walitoka Ujerumani, Eire, Uingereza na Uskoti, pamoja na Wachina waliotafuta kazi hasa Kalifornia. Baada ya mwaka 1880 hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914-1918) wengi walifika kutoka Ulaya ya Kusini na Mashariki, hasa Waitalia, Wayahudi kutoka Milki ya Urusi, Wapolandi na wenyeji wa nchi nyingine za Kislavi. Wahamiaji hao walileta pia tamaduni zao na kukubali mishahara midogo kuliko wenyeji waliowahi kufika mapema; hali hiy ilileta mara kadhaa sheria zilizolenga kuweka mipaka; sheria ya 1882 ilikataa kufika kwa Wachina, sheria ya 1922 ililenga kupunguza idadi ya Waitalia, Wayahudi na watu wa Ulaya ya Mashariki kwa kutaja mipaka kwa kila nchi ya asili[1].

Katika siasa ya nje, Marekani iliwahi kutangaza tangu mwaka 1823 kwamba ilitazama Amerika yote kama eneo ambako haikubali kuingiliwa na nchi za Ulaya; wakati ule koloni nyingi za Amerika ya Kusini zilikuwa zikifaulu kupata uhuru kutoka Hispania, na Marekani ilitaka kusisitiza isingekubali kuingia kwa mataifa mengine ya Ulaya.

Katika miongo iliyofuata uchumi wa Marekani uliimarishwa pamoja na kukua kwa sekta ya viwanda na wafanyabiashara wa Marekani walipanua biashara yao kimataifa; mnamo 1854 manowari za Marekani ziliilazimisha Japani kukubali kufunguliwa kwa ubalozi na kupokea wafanyabiashara. Meli za wafanyabiashara wa Marekani zilifika kote duniani, tangu miaka ya 1830 hadi Zanzibar ambako ubalozi mdogo ulifunguliwa mwaka 1837[2]. Wakati wa vita dhidi ya Hispania Marekani ilihakikisha pia nafasi yake katika bishara ya China dhidi ya mipango ya mataifa ya Ulaya ya kuigawa nchi hiyo.

Mwaka 1917 Marekani iliingia katika Vita Kuu ya Kwanza upande wa Uingereza na Ufaransa; baada ya vita rais Woodrow Wilson alishawishi mataifa mengine kuanzisha Shirikisho la Mataifa lakini bunge lilizuia kuingia kwa Marekani katika umoja huo.

Mdodoro mkuu wa mwaka 1929 ulileta matatizo makubwa kwa uchumi na hata njaa kwa raia wengi lakini ulileta pia siasa mpya ya "New Deal" chini ya rais Franklin D. Roosevelt ambako mara ya kwanza programu za kisiasa zilitumia mapato ya serikali kwa shabaha ya kusaidia idadi kubwa ya wananchi waliokuwa bila kazi, bila nyumba na bila mapato; vijana mamilioni waliajiriwa na serikali kwa kazi ya kujenga miundombinu (barabara, mifereji) na kuboresha hifadhi za taifa.

Mwaka 1941 Marekani iliingia katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia baada ya kushambuliwa na Japani na kupokea tangazo la vita kutoka Ujerumani. Uwezo wa kiuchumi wa Marekani uliwezesha ushindi wa mataifa ya ushirikiano. Uwezo wake wa kisayansi ulipanushwa na wanasayansi kama Albert Einstein waliopaswa kukimbia udiketa wa Hitler katika Ujerumani na kuiwezesha kutengeneza mabomu ya kwanza ya nyuklia yaliyotumiwa 1945 pale Hiroshima na Nagasaki.

Katika miongo ya vita baridi iliyofuata, Marekani ilikuwa taifa la kuongoza nchi zenye demokrasia na pia zile ambazo zilisimama upande wa ubepari tu bila demokrasia dhidi ya nchi za kikomunisti zilizoongozwa na Umoja wa Kisovyeti.

Mwanzo wa miaka ya 1960 ilishindana na Umoja wa Kisovyeti katika mbio wa kuingia katika anga-nje ikafaulu kupeleka watu wa kwanza hadi Mwezi mnamo 1969. Kutokana na ushindani wa Marekani na nchi za ukomunisti Marekani iliingia katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Vietnam hadi kushindwa pale mwaka 1975.

Vilevile miaka ya 1960 ilikuwa kipindi cha mapambano kwa ajili ya haki za watu weusi, wajukuu wa watumwa wa awali hasa katika kusini ya Marekani. Sheria zilizotenganisha watu pamoja na matumizi ya shule, vyuo, majengo na taasisi za burudani kulingana na rangi ya ngozi, zilizozuia ndoa kati watu wa rangi tofauti na kuzuia watu maskini wasitumie haki za kiraa zilipigwa marufuku bila kuondoa tofauti katika uwezo wa kiuchumi kati ya makundi katika jamii.

Mapinduzi ya kiteknolojia ya kompyuta na intaneti yalienea hapa haraka kushinda sehemu nyingine za Dunia.

Watu

Nchi ina wakazi zaidi ya milioni 320, na ina mchanganyiko mkubwa wa asili kuliko nyingine yoyote duniani.

Lugha

Ingawa Muungano hauna lugha rasmi, majimbo yake 32 yanaipa hadhi hiyo lugha ya Kiingereza, iliyo lugha ya kwanza kwa asilimia 80 ya wakazi.

Wakazi wengine wanatumia lugha nyingine nyingi, hasa kulingana na nchi ya asili ya ukoo wao. Kati ya lugha hizo, inaongoza kwa mbali ile ya Kihispania (12%).

Dini

Nchini dini zote zina uhuru mkubwa, tena kwa asilimia 59 ya wakazi dini ina umuhimu wa hali ya juu, tofauti na nchi tajiri nyingine duniani.

Asilimia 70.6 hivi ya wakazi wanafuata Ukristo katika mojawapo ya madhehebu yake, hasa ya Uprotestanti (46.5%), ingawa ile kubwa zaidi ni Kanisa Katoliki (20.8%).

Dini nyingine zina asilimia 4.7, na kati yake inaongoza ile ya Uyahudi (1.9%), ikifuatwa na Uislamu (0.9%).

Watu maarufu

Tazama pia

Marejeo

Tanbihi

  1. Closing the door on immigration, tovuti ya national Park service, Marekani, iliangaliwa Oktoba 2020
  2. Gilbert, Wesley. Our Man in Zanzibar: Richard Waters, American Consul (1837-1845), tasnifu 2011 kwenye Wesleyan University, Middletown, Connecticut online hapa

Viungo vya Nje

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
  • Official U.S. Government Web Portal Gateway to government sites
  • House Official site of the United States House of Representatives
  • Senate Official site of the United States Senate
  • White House Official site of the President of the United States
  • [[[:Kigezo:SCOTUS URL]] Supreme Court] Official site of the Supreme Court of the United States
Historia
Ramani
Vingine


Majimbo na maeneo ya Marekani
Majimbo ya Marekani
AlabamaAlaskaArizonaArkansasCaliforniaColoradoConnecticutDelawareFloridaGeorgiaHawaiiIdahoIllinoisIndianaIowaKansasKentuckyLouisianaMaineMarylandMassachusettsMichiganMinnesotaMississippiMissouriMontanaNebraskaNevadaNew HampshireNew JerseyNew MexicoNew YorkNorth CarolinaNorth DakotaOhioOklahomaOregonPennsylvaniaRhode IslandSouth CarolinaSouth DakotaTennesseeTexasUtahVermontVirginiaWashingtonWest VirginiaWisconsinWyoming
Mkoa wa Mji Mkuu
Mkoa wa Columbia (Washington D.C.)
Visiwa vya ng'ambo
Katika Pasifiki: Samoa ya MarekaniVisiwa vya Mariana ya KaskaziniGuamKatika Karibi: Puerto RicoVisiwa vya Virgin vya MarekaniVisiwa vidogo sana vya Pasifiki:Kisiwa cha HowlandKisiwa cha Jarvis Atolli ya JohnstonKingman ReefAtolli ya MidwayKisiwa cha BakerAtolli ya PalmyraKisiwa cha WakeKisiwa kidogo cha Karibi: Kisiwa cha Navassa
Makala hii kuhusu maeneo ya Marekani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Marekani kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.