Kipoland

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lugha ya Kipoland
Kinazungumzwa katika: Poland (38.5 milioni); Pia kuna wanzungumzaji katika Australia, Kanada, Uingereza, Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Belarus, Lithuania, Ukraine, Argentina, Brazil, Israel, na nchi nyingine kibao.
Waongeaji: zaidi ya milioni 50
Kama lugha rasmi:
Nchi: Poland
Uianishaji wa kiisimu:
Lugha za Kihindi-Kiulaya
   Lugha za Kislavoni
      Kislavoni cha Magharibi
         Lugha za kilekhi
            Lugha ya Kipoland

Kipoland (język polski, polszczyzna) ni lugha rasmi kwa nchi ya Poland. Kinafahamika zaidi kwa kuzungumzwa na watu waishio Maghari mwa Slovoni na ni lugha ya pili kwa ukubwa katika orodha ya Lugha za Kislavoni baada ya Kirusi. Ni moja kati ya lugha ngumu kujifunza kutokana na ugumu wa sarufi zake.

Katika historia, Kipoland kilikuwa lugha muhimu katika Ulaya ya Kati na Mashariki. Leo hii, kinazungumzwa na zaidi ya watu milioni 38.5 ikiwa kama lugha rasmi katika Poland. Pia kinazungumzwa kama lugha ya pili katika sehemu za magharibi mwa nchi ya Belarus, Lithuania, na Ukraine.

Kutokana na kuhamahama kwa watu wa Poland wa majira tofauti, mamilion ya waongeaji wa Kipoland wanaweza kupatikana katika nchi nyingi tu kama vile Australia, Kanada, Uingereza, Marekani, na sehemu nyingine nyingi tu. Kuna zaidi ya milioni 50 ya waongeaji wa Kipoland duniani.

Herufi[hariri | hariri chanzo]

Kuna takriban herufi 9 za Kipoland ambazo katika Kiingereza hakuna. Zinaonekana kuwa kama Kiingereza, lakini zenyewe zinaviji alama kwa juu au kwa chini.

Katika herufi ndogo, herufi tisa ni: ą ć ę ł ń ś ó ź ż

Katika herufi kubwa, herufi tisa ni: Ą Ć Ę Ł Ń Ś Ó Ź Ż

Kuna herufi 3 katika Kiingereza ambazo katika Kipoland hazitumiki: q, v, x.

Kuna mchanganyiko wa herufi 7 katika kila herufi 2 ambazo zote zinaonekana kuwa kama sawa katika kusikika (ambazo sawa na "th" au "qu" katika Kiingereza). Ambazo zimejumlisha herufi kama vile "ch", "cz", "dz", "dź", "dż", "rz", "sz".

Kusikika[hariri | hariri chanzo]

Lafudhi[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya Kipoland ina lafudhi nyingi sana, lakini ni chache mno kuliko lugha zingine za Ulaya. Kuna utofauti mdogo tu katika Kipolanda cha "kawaida", lakini kila mwongeaji anaweza kumwelewa mwenziwake, na wale ambao wao sio wazawa wa lugha hiii kawaida hawezi kujua tofauti zao katika kutamka.

Maneno kadhaa ya Kipoland[hariri | hariri chanzo]

ja - mimi
ty - wewe
on - yeye
my - sisi
oni - wao

co? - nini?
kto? - nani?
gdzie? - mahali gani?
dokąd? - wapi?
kiedy? - hini?
jak? - vipi?
dlaczego? - kwanini?
który? - ipi?

Namba:

moja - jeden
mbili - dwa
tatu - trzy
nne - cztery
tano - pięć
sita - sześć
saba - siedem
nane - osiem
tisa - dziewięć
kumi - dziesięć
kumi na moja - jedenaście
kumi na mbili - dwanaście
ishirini - dwadzieścia
ishirini na moja - dwadzieścia jeden
thelathini - trzydzieści
arobaini - czterdzieści
hamsini - pięćdziesiąt
mia moja - sto
elfu moja - tysiąc

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]