Kirusi
Kirusi ( русский язык russkii yazik) ni moja kati ya lugha za Kislavoni cha Mashariki yenye wasemaji wengi kati ya lugha zote za Kislavoni. Kirusi huandikwa kwa lugha alfabeti ya Kikyrili.
Kirusi ni lugha rasmi katika Urusi na pia lugha rasmi katika nchi jirani za Belarus, Kazakhstan na Kirgizia. Wasemaji wa Kirusi wako katika nchi zote zilizokuwa sehemu ya Umoja wa Kisovyeti hadi 1991. Kuna pia Warusi katika nchi za magharibi kwa sababu wakati wa ukomunisti palikuwa na wakimbizi waliotoka nje ya Urusi kwa sababu za kisiasa.
Watu wengi duniani wamejifunza Kirusi kwa sababu ilikuwa lugha ya kimataifa kati ya nchi zilizoshikamana na Umoja wa Kisovyeti. Wanafunzi wengi kutoka nchi mbalimbali za Afrika walipata elimu ya juu kwenye vyuo vikuu vya Umoja wa Kisovyeti kwa lugha ya Kirusi.
Viungo vya Nje [hariri]
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.