Siasa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Siasa[hariri | hariri chanzo]

Siasa ni njia ya kufanya maamuzi katika taifa, mji au hata dunia nzima (siasa ya kimatatifa). Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.

Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, na kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kujadiliana kuhusu maamuzi.

Mifumo ya Siasa[hariri | hariri chanzo]

Hapo chini, mifumo mingine ya kisiasa huelezwa kifupi:

==Utawala wa Kifalme== ni mfumo wa kiuongozi unaompa mamlaka ya dola na serikali Mfalme. Katika mfumo huu madaraka hurithiwa na familia ya kifalme. ==Utawala wa Kiimla== ni mfumo wa kiuongozi unaotoa madaraka yasiyo na mipaka kwa kiongozi. Katika utawala huu watu binafsi hawana haki na uhuru wa kimaamuzi. ==Utawala finyu== ni mfumo unaowapa wachache nguvu za maamuzi katika dola na serikali.Nafasi ya wachache hawa hutokana na haiba na uwezo wao kiuchumi, kijamii, kijeshi au kutokana na mafanikio yao katika nyanja mbalimbali za maisha. Mfumo huu ni nadra sana katika siku za hivi karibuni. Pia waweza kuitwa utawala wa makabaila. ==Utawala wa Umma== ni utawala unaotokana na jamii kuamua misingi ya kujiongoza. Mfumo huu wa utawala hujulikana kama Utawala wa Kidemokrasia na umegawanyika katika sehemu nne. ==Demokrasia Baguzi== ni aina ya Demokrasia inayojikita katika kulinda nguvu za kiuchumi zaidi. ==Demokrasia Duni== ni aina ya demokrasia inayotokana na makundi ya watu na kisha kupitia makundi hayo watu kuunda serikali mf- chama - serikali. ==Demokrasia Endelevu== ni aina ya demokrasia inayotoa fursa ya usawa na kupinga matabaka katika jamii. ==Demokrasia Shirikishi== - Katika aina hii ya Demokrasia wachache hupewa dhamana na wengi katika uwakilishi wa jamii katika maamuzi. ==Demokrasia== ni mfumo unatoa fursa ya madaraka kwa umma moja kwa moja au kutokana na kuwakilishwa.