Hisabati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Euklides, mwanahisabati wa Ugiriki wa Kale, karne ya 3 KK, alivyochorwa na Raffaello Sanzio.[1]

Hisabati ni somo linalohusika na idadi, upimaji na ukubwa wa vitu.

Kwa ujumla linahusika na miundo na vielezo.

Hisabati linaundwa na masomo mbalimbali, kama hesabu, jiometria na aljebra.

Neno hisabati katika lugha ya Kiswahili limetokana na neno la Kiarabu حسابات (halisi: hesabu (wingi)).

Somo hili huweza kutumika kutatua matatizo mbalimbali, lakini hasa ni la msingi katika uelewa wa ulimwengu kisayansi. Hivyo hutumiwa na masomo mengine kama Fizikia, Jiografia, Kemia katika mafunzo yake.

Mantiki ya kihisabati Nadharia ya seti Nadharia ya kategoria Nadharia ya kuhesabu

Historia ya Hisabati

Mwanahisabati Mjerumani Carl Friedrich Gauss aliita hisabati malkia wa sayansi ambayo inasaidia katika uvumbuzi wa kisayansi. Somo la hisabati lilikita mizizi kwa sababu ya uchu wa wanasayansi kupenda kutatua shida kama vile za biashara, ugavi wa ardhi na masomo ya sayari na katika kukisia uzani.

Tanbihi

  1. No likeness or description of Euclid's physical appearance made during his lifetime survived antiquity. Therefore, Euclid's depiction in works of art depends on the artist's imagination (see Euclid).

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hisabati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.