Kimalta
Kimalta ni lugha rasmi kwenye nchi ya kisiwani ya Malta katikati ya Bahari ya Mediteranea. Kimalta huhesabiwa kati ya lugha za Kisemiti ikiwa ni lugha pekee ya familia hiyo katika nchi za Ulaya.
Kimalta ni karibu na Kiarabu cha Tunisia lakini huandikwa kwa alfabeti ya Kilatini. Lugha imepokea maneno mengi kutoka Kiitalia na Kiingereza. Siku hizi takriban nusu ya maneno yana asili ya Kiitalia, na theluthi moja ni Kiarabu. Mengine yameingia kutoka kwa Kiingereza. Misingi ya sarufi ni Kiarabu.
Yaliyomo |
Historia [hariri]
Asili ya lugha ni visiwa kuvamiwa na Waarabu Waislamu mwaka 870. Hao walitawala hadi 1091 na katika kipindi hiki lugha ya Kiarabu ilienea kisiwani.
Baada ya Ufalme wa Wanormandi wa Sisilia kupata utawala wa funguvisiwa ya Malta, watawala wapya walivumilia lugha ya Kiarabu.
Katika karne zilizofuata Kimalta kikaendelea kujenga tabia za pekee na maendeleo ya Kiarabu barani.
Tangu karne ya 16 lugha ya kiutawala ilikuwa Kiitalia, lakini wakulima na wavuwi waliendelea na Kimalta.
Mwaka 1936 wakati wa utawala wa Waingereza Kimalta kilipewa hadhi ya lugha rasmi pamoja na Kiingereza badala ya Kiitalia.
Idadi ya wasemaji ni takriban watu 370,000.
Mifano ya maneno ya Kimalta [hariri]
Asili ya Kiarabu [hariri]
- wieħed („moja“) < واحد wāḥid
- kbir („kubwa“) < كبير kabīr
- raġel („mwanaume“) < رجل raǧul
- ħobż („mkate“) < خبز ḫubz
- qamar („mwezi“) < قمر qamar
- belt („mji“) < بلد balad
- id („mkono“) < يد yad
- tajjeb („njema“) < طيب ṭayyib
- saba' („kidole“) < إصبع ʾiṣbaʿ
- sema („anga“) < سماء samāʾ'
- marid („mgonjwa“) < مريض marīḍ
- tqil („nzito“) < ثقيل ṯaqīl
- xahar („mwezi“) < شهر šahr
- tifla („binti“) < طفلة ṭifla
- kelma („neno“) < كلمة kalima
- marsa („bandari“) < مرسى marsan
Asili ya Kiitalia [hariri]
- gravi („muhimu“) < grave
- lvant („mashariki“) < levante
- skola („shule“) < scuola
- parti („sehemu“) < parte
- avukat (wakili) < avvocato
- natura („hali asilia“) < natura
- frotta („tunda“) < frutto
- griż („kijivu“) < grigio
Viambishi ni mofimu au viungo vyenye maana ambavyo hufungamanishwa na mzizi/shina la neno ili kulipa neno hilo maana mbalimbali za kisarufi kama vile nafsi, wakati, hali, urejeshi, n.k Viambishi awali ni vile vinavyotangulia mzizi wenyewe, yaani huwa kabla ya mzizi/shina. SHINA AU MZIZI: Hakuna tofauti kati ya shina na mzizi MZIZI/SHINA, Ni sehemu ya neno inayobeba maana yake kuu na huwa haibadiliki, Kwa mfano, tuangalie vitenzi vifuatavyo: a-na-LIM-a wa-li-LIM-i-a ni-ta-LIM-iw-a wa-na-vyo-LIM-a Ukiangalia kwa makini, utaona kuna sehemu ya kitenzi hiki ambayo haibadiliki katika mifano ya hapo juu. Sehemu hiyo ni (-LIM-). Na hii ndiyo shina au mzizi wa kitenzi LIMA. Mfano mwingine: a-li-ki-SOM-a hu-SOM-ew-a wa-li-SOM-e-an-a a-li-m-SOM-e-a i-li-SOM-w-a Tunaona hapa mzizi/shina la kitenzi SOMA, ni -som- Ili utambue shina/mzizi wa kitenzi unafaa kuwazia hali mbalimbali au kauli tofautitofauti za mnyambuliko wa kitenzi halafu ubainishe sehemu isiyobadilika.