Denmark

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kongeriget Danmark
Ufalme wa Denmark
Bendera ya Denmark Nembo ya Denmark
Bendera Nembo
Wito la taifa: hakuna
Wimbo wa taifa: Der er et yndigt land (kitaifa);
Kong Christian (kifalme)
Lokeshen ya Denmark
Mji mkuu Kopenhagen
55°43′ N 12°34′ E
Mji mkubwa nchini Kopenhagen
Lugha rasmi Kidenmark1
Serikali Ufalme wa kikatiba
Margrethe II
Helle Thorning-Schmidt
Kuungana kwa nchi
{{{established_events}}}
mnamo 980 BK
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
43,094 km² (ya 1341)
1.6%1
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - 2006 sensa
 - Msongamano wa watu
 
5,431,000 (ya 109)
5,450,661
126/km² (ya 783)
Fedha Kroner (DKK)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET3 (UTC+1)
CEST3 (UTC+2)
Intaneti TLD {{{cctld}}}
Kodi ya simu +453
1 Habari zote za Denmark bila Faroe na Greenland.


Ramani ya Denmark

Denmark (pia Denmaki (au Denimaki au Denmak) - Kidenmark: Kongeriget Danmark) ni ufalme ya Ulaya ya Kaskazini. Ni nchi ndogo kati ya nchi za Skandinavia. Imepakana na Ujerumani kwa kusini na kuzungukwa na maji pande tatu. Kaskazini yake iko Unowe ng'ambo ya mlango wa bahari ya Skagerak, mashariki iko Uswidi ng'ambo ya Kattegat na Oresund. Bahari ya Kaskazini iko upande wa magharibi, Baltiki inaanza kwenye visiwa vikuu vya Denmark.

Eneo[hariri | hariri chanzo]

Denmark ina eneo la 43.000 km². Theluthi ya eneo hili ni kwenye visiwa 443 vya Denmark ambavyo 76 kati vyao vinakaliwa na watu.

Rasi ya Jutland ni sehemu kubwa ya eneo. Jutland ni Denmark bara. Ina urefu wa 300 km kuelekea kaskazini kutoka mpaka wa Ujerumani hadi ncha yake kwa Skagen.

Kwa jumla Denmark iko tambarare. Mlima wa juu ina kimo wa 170 m juu ya UB pekee.

Visiwa vikubwa ni Funen (Fyn), Zealand (Sjælland) na Bornholm (Bornholm).

Greenland na visiwa vya Faroe ni sehemu ya ufalme wa Denmark lakini zinajitawala.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu ya: Historia ya Denmark

Wadenmark wa kwanza waliojulikana katika historia kwa jina ni makabila ya Wakimbri na Wateutonia waliohamia hadi Ulaya ya kusini wakati wa njaa mnamo mwaka 113 KK.

Katika karne za 8 hadi ya 11 BK majambazi wa baharini kutoka Denmark na Norway waliogopwa kote Ulaya kwa jina la "Waviking". Walivamia pia Uingereza mara kwa mara na kujenga makao huko. Tangu mwaka 793 walitawala eneo la Danelag (au: Danelaw) iliyoenea katika kaskazini na kaskazini-mashariki ya Uingereza wa leo.

Katika karne ya tisa na karne ya kumi maeneo madogo yaliunganishwa. Wafalme wa kwanza wanaojulikana kutawala Denmark yote walikuwa Garm Mzee na Harald Jino Buluu (mnamo mwaka 980 BK). Harald alikuwa mfalme wa kwanza wa kupokea Ukristo wa kikatoliki. Denmark ikawa nchi yenye nguvu katika Skandinavia na kwenye pwani za Baltiki.

Kati ya 1397 hadi 1521 nchi zote za Skandinavia ziliunganishwa katika maungano ya kifalme chini ya wafalme wa Denmark ilhali kila nchi ilijitawala katika mambo ya ndani. Baada ya Uswidi kujitenga na umoja huu Norway iliendela kuwa chini ya Denmark hadi mwaka 1814.

Mwaka 1537 Denmark ilijiunga na mwendo wa Matengenezo ya Kanisa na kanisa la Kiluteri likawa dini rasmi nchini. Denmark ilikuwa kati ya nchi muhimu sana ya Uluteri.

Baada ya vita za Napoleoni Denmark iliondolewa utawala wa Norway iliyounganishwa na Uswidi mwaka 1814. Lakini koloni za Greenland, Iceland, Faroe na visiwa vya Karibi zilibaki kwa nchi.

Karne ya 19 ilileta fitina na Ujerumani juu ya utawala wa Schleswig na Holstein. Baada ya vita ya 1864 Denmark ilipaswa kuacha majimbo haya mawili kwa Ujerumani.

Denmark haikushiriki katika Vita Kuu ya Dunia ya Kwanza lakini ilirudishwa sehemu ya kaskazini ya jimbo la Schleswig.

Wakati wa Vita Kuu ya Dunia ya Pili Denmark ilivamiwa na Ujerumani mwaka 1940 hadi 1945. Wakati wa vita Iceland iliamua kutangaza uhuru wake. 1948 mara baada ya vita visiwa vya Faroe vilipewa madaraka ya kujitawala lakini vilibaki ndani ya umoja na Denmark. Koloni ya Greenland ilipewa madaraka haya mwaka 1979.

Denmark ikawa kati ya nchi zilizounda UM na pia NATO. Mwaka 1973 ikajiunga na Jumuiya ya Ulaya (sasa: Umoja wa Ulaya).

Waja[hariri | hariri chanzo]


Nchi za Umoja wa Ulaya Bendera ya Umoja wa Ulaya
Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi
Europa Mapa.png Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Denmark kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.