Walutheri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Lebo ya Luther: msalaba, moyo na waridi

Walutheri ni jina linalotumika kuwataja kwa jumla wafuasi wa Yesu Kristo wanaozingatia mafundisho yaliyotolewa na Martin Luther katika Karne ya 16.

Idadi yao ni kama milioni 60, walioenea hasa Ujerumani, Skandinavia na Marekani; katika bara la Afrika wako hasa Ethiopia na Tanzania.

Ingawa wamegawanyika katika makanisa mengi hasa ya kitaifa, tangu mwaka 1947 wameunda shirikisho la kimataifa linalounganisha wengi wao.

Msingi wao ni Biblia ya Kikristo yenye vitabu 66.

Wanaadhimisha sakramenti 2, yaani Ubatizo na Chakula cha Bwana.