Agano la Kale

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Agano la Kale ni mkusanyo wa vitabu vya sehemu ya kwanza ya Biblia inayotumiwa na waumini wa Ukristo duniani. Pengine mkusanyo huu unagawanywa katika makundi ya sheria, historia, ushairi, na unabii, ambayo ni tofauti kiasi na kawaida ya Tanakh ya Uyahudi wa leo.

Vitabu vyote vya Agano la Kale viliandikwa kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Kwa mujibu wa wanahistoria wa Biblia, vitabu vya Agano la Kale viliandikwa kati ya karne ya 11 KK na karne ya 1 KK.

Yaliyomo

[hariri] Orodha tofauti za vitabu vya Agano la Kale

Katika mapokeo ya Kikristo kuna orodha tofauti za vitabu vya Agano la Kale. Hasa kuna matoleo yenye vitabu 39 na kuna matoleo yenye vitabu 46.

  • Waprotestanti wengi hukubali vitabu 39 ambavyo ni sawa na Tanakh ya Kiyahudi.
  • Wakatoliki hukubali vitabu 46 yaani hivyo 39 na 7 vingine (Deuterokanoni) ambavyo ni: Yuditi, Tobiti, Yoshua bin Sira, Hekima, 1 Wamakabayo na 2 Wamakabayo, halafu sehemu za nyongeza za vitabu vya Danieli na Esta.
  • Baadhi ya Waorthodoksi wana vitabu vingine pia kama vile Esra 1 (Esra ya Kiebrania huhesabiwa kama Esra 2), 3 Wamakabayo na zaburi 151; kama nyongeza 4 Wamakabayo; Ufunuo wa Esra na hata vingine.

[hariri] Biblia ya Kiebrania au Biblia ya Kigiriki?

Asili ya mahesabu haya mawili ni hasa desturi tofauti ndani ya Uyahudi wakati wa Yesu na karne mbili za kwanza BK. Kanuni ya Biblia ilikuwa haijafungwa wakati ule. Hivyo palikuwa na mikusanyo tofauti kati ya Wayahudi wenye lugha ya Kiebrania au ya Kiaramu kwa upande mmoja na Wayahudi waliotumia lugha ya Kigiriki kwa upande mwingine.

Wayahudi wenye lugha ya Kigiriki (waliokaa nje ya Palestina, hasa katika nchi mbalimbali za Dola la Roma na kuzidi idadi ya Wayahudi katika Palestina Israeli penyewe) walitumia toleo la Kigiriki la Septuaginta. Wakristo wa kwanza walizoea toleo hilo hasa kwa sababu lugha ya mawasiliano kati ya Wakristo ilikuwa Kigiriki kama lugha ya kimataifa. Ndiyo sababu Agano Jipya lote liliandikwa kwa Kigiriki.

Upande wa Uyahudi uamuzi kuhusu vitabu vinavyofaa kuhesabiwa kuwa sehemu za Biblia ya Kiebrania lilifanywa kati ya miaka 80 - 135 BK ambapo wataalamu Wayahudi waliamua kukubali vitabu vile tu vilivyotunzwa kwa Kiebrania. Hivyo maandiko kadhaa zisizoandikwa kwa Kiebrania vilifungwa nje. Sababu mojawapo ya uamuzi wao ilikuwa kubishana na Wakristo waliovitumia.

Jumuia za Kiyahudi zilipokea uamuzi huo lakini Wakristo waliendelea kutumia Septuaginta, iliyotafsiriwa baadaye kwa Kilatini na lugha nyingine za mataifa na makabila yaliyopokea imani ya Kikristo.

Hivyo Biblia ya Wakristo ulikuwa na vitabu vya Septuaginta hadi matengenezo ya Kanisa katika karne ya 16.

Martin Luther alianza kutafsiri Biblia upya kutoka lugha asilia akaona achague vitabu vyake, akinyofoa 7 vya Agano la Kale pamoja na 7 vya Agano Jipya kadiri alivyoviona kuwa na mafundisho sahihi kiimani. Hivyo upande wa Agano la Kale alilingana na Wayahudi na kutofautiana na jinsi ilivyokuwa kawaida katika Kanisa Katoliki ambalo katika Mtaguso wa Trento (karne ya 16) lilithibitisha matumizi ya vitabu 46 katika Agano la Kale.

Tangu Luther matoleo mengi ya Kiprotestanti huonyesha vitabu vya Agano la Kale kuwa 39. Mara nyingine vitabu 7 vya Deuterokanoni vinaongezwa baada ya Agano la Kale kama sehemu ya pekee vikiitwa "Apokrifa".

[hariri] Vitabu vya Agano la Kale

Orodha hii inafuata kawaida ya Wakristo walio wengi. Umbo la majina ni ule wa "Biblia - Habari Njema kwa Watu Wote". Vitabu saba vinafuatwa na alama ya DK ni vile ambavyo huhesabiwa kando na Waprotestanti wengi kama "Apokrifa" lakini hutazamiwa kama vitabu kamili vya Biblia (Deuterokanoni) katika mapokeo ya Kanisa Katoliki na ya Waorthodoksi wengi.

[hariri] Vitabu vya Kihistoria

  • 1. Vitabu vitano vya Torati vinavyoitwa pia "vitabu vya Musa":

[hariri] Vitabu vya Kishairi au vya hekima

[hariri] Vitabu vya manabii

[hariri] Viungo vya nje

Image:WikiLettreMini.svg Makala hiyo kuhusu "Agano la Kale" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri".

Ikiwepo makala kuhusu Agano la Kale kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili.

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Maamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia Esta TobitiDK YuditiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK Yoshua bin SiraDK Wimbo Ulio Bora Isaya Yeremia BarukDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Vifaa binafsi