Kitabu cha Ezekieli
Kati ya manabii muhimu zaidi wa Agano la Kale, mmojawapo ni Ezekieli, aliyefanya kazi miaka 592-570 hivi K.K., kadiri ya ushahidi wa kitabu chake.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
[hariri] Mazingira
Baada ya maangamizi ya Yerusalemu, polepole Wayahudi waliohamishiwa Babeli waliweza kujitafutia kazi (kwanza kilimo, halafu biashara), wakafaulu sana, hata wengine wakawa watumishi wa serikali.
Lakini upande wa dini walikuwa hatarini, kwa sababu imani ya Mwisraeli inategemea taifa, nchi na hekalu ambavyo vyote vilikuwa vimeharibika.
Kwa ajili yao Mungu akatuma tena manabii, hasa Ezekieli ambaye anaonekana kuwa alihamishwa tangu mwaka 598 K.K.
[hariri] Kazi ya Ezekieli
Akiwa kuhani, kama vile nabii Yeremia, katika kitabu chake alishughulika sana na hekalu na mambo ya ibada.
Upande mwingine alianzisha mtindo mpya wa kinabii ambao unaitwa wa Kiapokaliptiko (kilele chake ni Ufunuo wa Yohane) na ambao hauhusu tena matukio madogomadogo ya siasa, bali kwa njozi za ajabuajabu unaonyesha maana ya historia yote.
Katika maandiko yake njozi zinachukua nafasi kubwa na kwa mafumbo yake yanavutia ubunifu wetu ujitahidi kuelewa yaliyofichika katika mifano, tarakimu, rangi n.k.
Ezekieli alifundisha pia mambo mapya kama vile kwamba watu wanahitaji kufanywa upya hasa moyo na roho (11:17-20; 36:26) na kwamba Mungu anaamua kuwaokoa kabla hawajatubu ili jina lake litukuzwe katika watu wake: wokovu anaouleta hautegemei matendo mema ya binadamu, bali muungano wa Mungu na wale walioitwa kwa jina lake (16:58-63).
Hakuna kitabu kingine katika Biblia kinachosisitiza utukufu wa Mungu kuliko hicho.
Sura ya dini ya Uyahudi mpaka leo inategemea sana kazi aliyoifanya Ezekieli ya kukaza utekelezaji wa Torati hata pasipo uhuru wa kisiasa.
[hariri] Viungo vya Nje
Kitabu cha Ezekieli katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)
Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.