Kitabu cha Sefania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kitabu cha Sefania ni kimojawapo kati ya vitabu vya Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), hivyo kinapatikana pia katika Agano la Kale ambalo ni sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Kutokana na ufupi wake kimepangwa tangu kale kati ya vitabu 12 vya Manabii Wadogo.

Yaliyomo

[hariri] Mhusika

Nabii Sefania, mtu wa Yerusalemu alihubiri (640-625 hivi K.K.) kwa nguvu mwanzoni mwa utawala wa mfalme Yosia, kabla huyo hajaanza urekebisho wake wa kidini uliofuata kuvumbua katika hekaluni maandiko ya Kumbukumbu la Sheria.

[hariri] Ujumbe

Pamoja na kutisha kwa matabiri yake, aliahidi wokovu kwa mabaki ya Israeli, akisema watakuwa watu maskini na walionewa (3:9-20).

Ndio mwanzo wa imani ya kuwa wapenzi wa Mungu ni hasa mafukara, atakavyosisitiza Yesu (Lk 6:20-21).

[hariri] Ufafanuzi

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

[hariri] Viungo vya Nje

Kitabu cha Sefania katika tafsiri ya Kiswahili (Union Version)

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo Kutoka Walawi Hesabu Kumbukumbu Yoshua Waamuzi Ruthu Samueli I Samueli II Wafalme I Wafalme II Mambo ya Nyakati I Mambo ya Nyakati II Ezra Nehemia TobitiDK YudithiDK Esta Wamakabayo IDK Wamakabayo IIDK Yobu Zaburi Methali Mhubiri Hekima DK SiraDK Wimbo Bora Isaya Yeremia Maombolezo BarukuDK Ezekieli Danieli Hosea Yoeli Amosi Obadia Yona Mika Nahumu Habakuki Sefania Hagai Zekaria Malaki - Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine