Kitabu cha Nahumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nabii Nahumu katika picha ya Waorthodoksi ya karne XVIII.

Kitabu cha Nahumu (kwa Kiebrania נחום, Nahum) ni kimojawapo kati ya vitabu 12 vya gombo la Manabii wadogo katika Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania) na kwa hiyo pia katika Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo.

Muda[hariri | hariri chanzo]

Kitarehe kinashika nafasi kati ya kile cha nabii Mika na kile cha Habakuki.

Mada[hariri | hariri chanzo]

Katika kitabu hiki Nabii Nahumu anashangilia kwa ufasaha wa ushairi ujio wa maangamizi ya dola la Waashuru na ya makao yao makuu, Ninawi (612 KK): hivyo adui wa taifa na wa Mungu hatimaye ataadhibiwa.

Mtunzi[hariri | hariri chanzo]

Mtunzi anadhaniwa kuwa nabii wa Yerusalemu wakati wa mfalme Yosia wa nchi ya Yuda.

Ufafanuzi[hariri | hariri chanzo]

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Nahumu kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.