Deuterokanoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Vitabu vya deuterokanoni (kutoka Kigiriki "deuteros" = ya pili na "kanon" = orodha[1]) ni maandiko yanayotazamwa na Wakatoliki, na baadhi ya Waorthodoksi na ya Makanisa ya Kale ya Mashariki kama sehemu kamili ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo[2].

Vitabu hivyo viliandikwa miaka 300 - 50 KK[3][4][5].

Wayahudi na Waprotestanti wengi huviita apokrifa na kuvitazama kama vitabu vinavyostahili kuheshimiwa lakini si sawa na Biblia yenyewe[6].

Vitabu vya deuterokanoni vya Agano la Kale[hariri | hariri chanzo]

Katika Biblia zinazotolewa na Kanisa Katoliki ni vitabu saba vifuatavyo (pamoja na sehemu za vitabu vya Kitabu cha Esta na Kitabu cha Danieli):

Baadhi ya Waorthodoksi wana vitabu vingine pia kama vile Kitabu cha kwanza cha Ezra (Ezra ya Kiebrania huhesabiwa kama Ezra 2), Kitabu cha tatu cha Wamakabayo na Zaburi ya 151; kama nyongeza Kitabu cha nne cha Wamakabayo; Ufunuo wa Ezra na hata vingine.

Vitabu hivyo vyote ama havikuandikwa (Bar, 2 Mak, Hek) ama havikupatikana mapema kwa lugha ya Kiebrania (asili kwa Sir, Judt, 1Mak) wala ya Kiaramu (asili kwa Tob), bali kwa Kigiriki tu.

Historia ya orodha ya vitabu vya deuterokanoni[hariri | hariri chanzo]

Hadi karne ya 1 KK orodha ya vitabu vya Biblia ya Kiebrania ilikuwa haijaamuliwa, ingawa ilikuwa wazi ya kwamba vitabu vya Torati ni maandiko matakatifu kamili; katika suala la vitabu vingine Wayahudi bado walitofautiana, k.mf. Masadukayo walikataa hata vile vya Manabii vilivyokubaliwa na Mafarisayo.

Sehemu kubwa ya Wayahudi nje ya Israeli na Mesopotamia walitumia toleo la Kigiriki lililoitwa Septuaginta ambalo lilitafsiriwa na wataalamu Wayahudi huko Misri katika karne ya 2 na ya 3 KK.

Kabla ya kukamilika kwa orodha ya vitabu vya Agano Jipya Septuaginta ilikuwa ndiyo Biblia ya Wakristo wa kwanza (ambao wengi wao hawakujua Kiebrania)[7][8].

Baada ya maangamizi ya Hekalu la Yerusalemu (70) na hasa katika karne ya 2 wataalamu Wayahudi, walipopatana juu ya mapokeo yao ili kujiimarisha dhidi ya Ukristo na ustaarabu wa kigeni, waliamua kutovikubali kama sehemu za Tanakh vitabu visivyopatikana kwa lugha ya Kiebrania.

Wakristo hawakufuata maazimio hayo ya Wayahudi, hivyo mwishoni mwa karne ya 2 Wakristo magharibi mwa Mediteranea walianza kutafsiri Septuaginta kwa Kilatini kilichokuwa lugha kuu kwao.

Matamko ya Kanisa Katoliki[hariri | hariri chanzo]

Vitabu vya Deuterokanoni vilihesabiwa rasmi kuwa sehemu ya Biblia hasa kuanzia Hati ya Damasi au De explanatione fidei, iliyotolewa na Papa Damasus I mwaka 382 [9].

Tafsiri ya Kilatini ya Hieronimo iliyoitwa Vulgata ilipata kuwa toleo muhimu katika Kanisa Katoliki. Hieronimo mwenyewe alipotafsiri Biblia upya katika Kilatini alisema vitabu vya Septuaginta kama Hekima, Yoshua bin Sira, Yudith na Tobiti havistahili kuwemo katika Biblia[10][11] lakini alivitafsiri ndani ya Vulgata kufuatana na maelekezo wa Papa Damaso I aliyemuagiza kazi [12]

Orodha hiyo ya Papa Damaso I ilipata nguvu Afrika Kaskazini kutokana na Agostino wa Hippo[13][14][15] kuifanya ipitishwe na Mtaguso wa Hippo (393), Mtaguso wa tatu wa Karthago (397) na Mtaguso wa nne wa Karthago (419)[16].

Wakati huohuo Papa Inosenti I aliituma kwa askofu Esuperi wa Toulouse (405)[17].

Baadaye Mtaguso wa Firenze (1442)[18] na Mtaguso wa Trento (1546)[19] ilivitambua rasmi kuwa sehemu za Biblia kamili kwa Kanisa Katoliki[20].

Misimamo ya Waprotestanti[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa Matengenezo ya kiprotestanti katika karne ya 16 Martin Luther na wengineo walishika msimamo mkali kuhusu kanuni ya Biblia akafuata azimio la Wayahudi na shauri la Hieronimo kuhusu vitabu hivyo.

Pamoja na hivyo waliweza kuweka pembeni hata baadhi ya vitabu vya Agano Jipya ambavyo zamani ulitokea wasiwasi juu yake na kwa sababu hiyo pengine vinaitwa pia deuterokanoni[21]:

Baada ya kifo cha Martin Luther, Waprotestanti kwa jumla walikubali tena vitabu vyote vya Agano Jipya[22] na kurudisha umoja katika jambo hilo la msingi kwa Ukristo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Bogaert, Pierre Maurice (2012). "The Latin Bible. c 600 to c. 900". In Richard Marsden; E. Ann Matter. New Cambridge History of the Bible; Vol II. Cambridge University Press. pp. 69–92. 
  2. Michael D., Coogan, ed. (2018). "The Canons of the Bible". The New Oxford Annotated Bible: New Revised Standard Version: An Ecumenical Study Bible (5th ed.). New York: Oxford University Press. pp. 1839, 1841. ISBN 978-0-19-027605-8. OCLC 1032375119. 
  3. Livingstone, E. A. (2013). The Concise Oxford Dictionary of the Christian Church (in English). OUP Oxford. pp. 28–29. ISBN 978-0-19-107896-5. Retrieved 17 June 2020. 
  4. Apocrypha. Wm. B. Eerdmans Publishing Co..
  5. Gleason L. Jr., Archer (1974). A Survey of Old Testament Introduction. Chicago, IL: Moody Press. p. 68. ISBN 9780802484468. Retrieved 7 October 2019. 
  6. The Popular and Critical Bible Encyclopædia and Scriptural Dictionary, Fully Defining and Explaining All Religious Terms, Including Biographical, Geographical, Historical, Archæological and Doctrinal Themes, p.521, edited by Samuel Fallows et al., The Howard-Severance company, 1901,1910. – Google Books
  7. J.N. D. Kelly, Early Christian Doctrines, p.53
  8. Stuart G. Hall, Doctrine and Practice in the Early Church, p. 28
  9. kwa Kilatini
  10. Edgecomb, Kevin P. (14 August 2006). Jerome's Prologue to Jeremiah. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-12-31. Iliwekwa mnamo 2021-07-11.
  11. Kelly, J. N. D. (1960). Early Christian Doctrines. San Francisco: Harper. p. 55. 
  12. "Hic prologus Scripturarum quasi galeatum principium omnibus libris, quos de hebraeo vertimus in latinum, convenire potest, ut scire valeamus, quicquid extra hos est, inter apocrifa seponendum. Igitur Sapientia, quae vulgo Salomonis inscribitur, et Iesu filii Sirach liber et Iudith et Tobias et Pastor non sunt canone. Macchabeorum primum librum hebraicum repperi, secundus graecus est, quod et ex ipsa φράσιν probari potest." (Hieronimo katika "Prologus Galeatus" au utangulizi kwa vitabu vya Samueli na Wafalme katika Vulgata)
  13. Everett Ferguson, "Factors leading to the Selection and Closure of the New Testament Canon," in The Canon Debate. eds. L. M. McDonald & J. A. Sanders (Hendrickson, 2002) p. 320.
  14. F. F. Bruce (1988), The Canon of Scripture. Intervarsity Press, p. 230.
  15. Augustine, De Civitate Dei 22.8
  16. McDonald & Sanders, editors of The Canon Debate, 2002, chapter 5: The Septuagint: The Bible of Hellenistic Judaism by Albert C. Sundberg Jr., p. 72, Appendix D-2, note 19.
  17. Westcott, Brooke Foss (2005). A general survey of the history of the canon of the New Testament (6th ed.). Eugene, OR: Wipf & Stock. p. 570. ISBN 1597522392. 
  18. Eccumenical Council of Florence and Council of Basel. Jalada kutoka ya awali juu ya 2016-02-20. Iliwekwa mnamo 2021-07-11.
  19. Paul III  Council of Trent-4. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-03-23. Iliwekwa mnamo 2021-07-11.
  20. ~The Council of Trent - Session 4~.
  21. James Akin, Defending the Deuterocanonicals, EWTN, archived from the original on 2019-07-16, retrieved 2021-07-11 
  22. Lutherbibel 1545. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-04-19. Iliwekwa mnamo 2021-07-11. note order: "...Hebräer, Jakobus, Judas, Offenbarung"; see also German Bible Versions.

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

  • Harrington, Daniel J. Invitation to the Apocrypha. Grand Rapids, Michigan: W.B. Eerdmans Publishing Co., 1999. ISBN 978-0-8028-4633-4
  • Roach, Corwin C. The Apocrypha: the Hidden Books of the Bible. Cincinnati, Ohio: Forward Forward Movement Publications, 1966. N.B.: Concerns the Deuterocanonical writings (Apocrypha), according to Anglican usage.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Deuterokanoni kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.