Torati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Gombo la Biblia kwa Kiebrania

Torati (kwa Kiebrania: תורה, Torah), maana yake ni fundisho, mwongozo au sheria. Kwa jina hilo vinatajwa kwa pamoja vitabu vitano vya kwanza vya Tanakh, vinavyojulikana pia kwa jina lenye asili ya Kigiriki la Pentateuko (pente maana yake tano, teukhos maana yake kitabu).

Kwa jina hilohilo Wayahudi wanamaanisha pia sheria ya dini yao kwa jumla, wakitofautisha Torah shebiktav (sheria iliyoandikwa yaani vitabu hivyo vitano) na Torah shebehalpeh kwa mapokeo yote yaliyokubalika baadaye. Kusoma Torah ni kati ya wajibu muhimu wa kila Mwisraeli. Ni desturi kusoma Torati nzima kwa mwaka mmoja, na kwa ajili hiyo imegawiwa sehemu 54 (parashoth, wingi wa parasha, yaani "sehemu"), kama zilivyo siku za Sabato katika miaka mirefu (yenye miezi 13).

Vitabu vitano vya Torati[hariri]

Vitabu vya Torah ni (majina ya vitabu kwa Kiebrania yanatokana na maneno yake ya kwanza):

Torati si mkusanyo wa mpango wa sheria, bali hasa msingi wa kiteolojia wa imani ya Israeli ("Mungu mmoja, taifa moja, nchi moja") ambamo zinapatikana sheria nyingi pia pamoja na historia ya taifa la Mungu. Sheria zinaweza zikafanana na zile za makabila ya jirani, lakini zina mambo ya pekee yanayotokana hasa na imani ya kuwa Mungu ni mmoja tu.

Mtazamo wa Wayahudi kuhusu Torah[hariri]

Torah ni msingi muhimu zaidi wa dini ya Kiyahudi na ya maadili yake yanatotegemea utekelezaji wa maagizo (mitzvot) 613.

Kadiri ya mapokeo yao vitabu hivyo vilitolewa na Mungu kwa Musa kwenye Mlima Sinai. Kwa hiyo hata herufi au ishara yake ndogo imewekwa na Mungu kama fundisho.

Wataalamu kuanzia mwisho wa karne ya 19 wameonyesha kuwa maandiko hayo yametokana na mapokeo mbalimbali, hasa manne yanaoitwa J, E, D na P.