Nchi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nchi ni sehemu ya dunia inayokaliwa na watu wa taifa moja chini ya serikali moja.

Nchi nyingi ziko barani lakini kuna pia nchi za visiwani. Eneo la nchi huwa pia na maji hasa ya bahari na asilimia ya uso wa bahari ni kubwa zaidi kama nchi ina visiwa vingi.

Kuna nchi kadhaa zilizopo kwenye bara zaidi ya moja.