Injili ya Mathayo
Injili ya Mathayo ni kitabu cha kwanza katika orodha ya vitabu vya Agano Jipya katika Biblia ya Ukristo.
Huhesabiwa kati ya Injili Ndugu pamoja na Marko na Luka, kwa sababu inafanana nazo kwa kiasi kikubwa; hasa inatumia asilimia 80 ya maandiko ya Marko.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Yaliyomo |
Mwandishi [hariri]
Katika matoleo ya Biblia kichwa cha kitabu ni "Injili kama ilivyoandikwa na Mathayo" lakini kichwa hiki si sehemu ya toleo asili la Kigiriki.
Ingawa Injili yenyewe haimtaji mwandishi wake, kuanzia Papias (mnamo mwaka 130) Mtume Mathayo ametajwa kama mwandishi wa misemo ya Yesu kwa lugha ya Kiebrania.
Wataalamu wanajadili kiasi gani maandishi yake yamechangia Injili hii jinsi ilivyo.
Muda wa uandishi [hariri]
Wakati wa kutolewa unaaminiwa na wataalamu wengi wa kisasa ilikuwa kati ya mwaka 80 na 90.
Tabia za Mathayo [hariri]
Mathayo anakazia kuwa Yesu wa Nazareti ndiye Masiya aliyetangazwa na manabii wa Agano la Kale. Kwa sababu hiyo Mathayo anaripoti maneno ya Agano la Kale mara kwa mara.
Tabia hii inachukuliwa kuthibitisha maelezo ya kwamba Injili hii ililenga Wakristo waliokuwa Wayahudi na kutumia lugha ya Kigiriki.
Mathayo anakazia pia mafundisho ya Yesu ilhali Marko anaeleza zaidi matendo yake.
Nembo ya Injili [hariri]
Injili hii inaanza kwa kuorodhesha mababu wa Yesu. Kutokana na mwanzo huu vizazi vya baadaye vilimpa Mwinjili Mathayo nembo la mwanamume au malaika akichora habari za Biblia.
Yaliyomo [hariri]
- Uzazi na utoto wa Yesu (Mat 1+2)
Uzazi wa Yesu, Kuzaliwa kwake, kukimbia Misri na mauaji ya watoto wa Bethlehemu - Chanzo cha kazi yake huko Galilaya (Mat 3-4)
Yohane Mbatizaji, Yesu ajaribiwa porini, Mitume ya kwanza - Hotuba mlimani (Mat 5-7)
- Uponyaji na miujiza (Mat 8 – 9,34)
- Mahubiri kuhusu wito la wanafunzi
Wito la mitume 12 (10,1-4), Tangazo la mateso yajayo (10,16-26), Hofu ya watu na kumhofia Mungu (10,26-33) - Mafundisho juu ya Yohane Mbatizaji, Wafarisayo na walimu wa sheria
- Mifano juu ya Ufalme wa Mungu (Mat 13)
Mfano wa mpanzi (13,1-9; maelezo 13,18-23), magugu katika ngano (13,24-30; maelezo 13,36-43), mfano wa mbegu wa haradali (13,31-32), chachu (13,33-35), hazina iliyofichika (13,44), lulu (13,45-46), wavu wa samaki (13,47-52) - Matendo mengine (Mat 13,53 - 17,27)
- Mahubiri na maaagizo kwa wanafunzi (Mat 18)
- Safari ya kwenda Yerusalemu (Mat 19-22)
- Mahubiri juu ya Yerusalemu, mateso yanayokuja na mwisho wa wakati (Mat 23-25)
- Mateso na ufufuo wa Yesu (Mat 26-28)
Kiungo cha nje [hariri]