Sinagogi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ukumbi wa sinagogi kisiwani Rhodos
Sinagogi ya Kale mjini Praha

Sinagogi ni nyumba ya kusali ya Wayahudi.

Yaliyomo

[hariri] Etimolojia

Neno latokana na Kigiriki συναγωγή sinagoge likimaanisha "mkutano"; ni tafsiri ya Kiebrania בית כנסת beit knesset yaani "nyumba ya mkutano". Wayahudi hutumia pia neno la Kiyiddish "shul" (=shule) kwa sinagogi.

[hariri] Muundo

Chumba kikuu ni ukumbi wa sala na mara nyingi kipo pamoja na vyumba vya pembeni kama vile madarasa, ofisi na vingine.

[hariri] Historia

Katika Israeli ya Kale kabla ya uvamizi wa Yerusalemu mwaka 587 KK hapakuwa na sinagogi wala hazitajwi kabisa katika Agano la Kale.

Hakuna uhakika kamili lakini inaonekana ya kwamba sinagogi zilianzishwa baada ya kubomolewa kwa hekalu ya Yerusalemu na uhamisho wa Wayahudi katika nchi za mbali.

Tangu kuharibiwa wa Hekalu ya Pili mwaka 70 Wayahudi walikuwa na masinagogi tu.

[hariri] Yaliyomo

Ukumbi wa sala huwa na sehemu zifuatazo:

  • sanduku la Torati ni kabati au sanduku ambako hati za kuviringisha zenye mwandiko wa Biblia hutunzwa.
  • taa inayoendelea kuwaka muda wote
  • meza ya msomaji ambako hati za torati hufunguliwa na kusomewa
  • mimbari ya mafundisho
  • kinara cha menorah chenye mishumaa 7 au 9
Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sinagogi kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.