Sala
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wanawake Wakristo wa Urusi wakisali pamoja
Mwanamume Mshinto wa Japani akisali peke yake
Sala ni njia ambayo binadamu anauelekea ulimwengu wa roho, hasa kwa lengo la kuongea na Mungu kwa sauti au kimoyomoyo.
Malengo yake yanaweza kuwa tofauti: kusifu, kushukuru, kuomba au kujiachilia.
Upande wa pili sala ni kutafakari ili kusikiliza na kuelewa ujumbe wa Mungu.
Sala inaweza kufanywa na mtu peke yake au na wengi pamoja, hata kwa kuimba.
Dini zinaelekeza waumini wake kusali kwa namna mbalimbali.
- Katika Uyahudi siku za kawaida kuna sala 3.
- Katika Ukristo inaheshimiwa sana liturujia ya mara kwa mara, lakini pia sala ya moyo.
- Katika Uislamu sala inatakiwa mara 5 kwa siku, ingawa zinahimizwa pia sala za hiari. Zulia inatumika kwa ajili ya kumsujudia Mungu.